November 24, 2024

Ijue mikoa kumi inayoongoza kwa mbuzi wengi Tanzania

Mikoa hiyo ni Arusha, Shinyanga, Geita, Mwanza, Simiyu, Tanga, Manyara, Singida, Dodoma na Mara ambayo yote kwa pamoja ina mbuzi zaidi ya milioni 13.

  • Takribani mbuzi milioni 13 kati ya milioni 19 waliopo Tanzania wanapatikani katika mikoa 10 tu. 
  • Mkoa wa Arusha unaongoza kwa kuwa na mbuzi wengi wanaofikia milioni 2.58.

Dar es Salaam. Mbuzi ni miongoni mwa wanyama wa kufugwa Tanzania ambao wanashika nafasi ya pili kwa wingi bara na visiwani .

Tanzania ina mbuzi zaidi ya milioni 19 ambapo milioni 18.94 sawa na asilimia 99.4 ya wanapatikana Tanzania bara na waliobaki sawa na asilimia 0.6 wanapatikana Zanzibar .

Mikoa ya Arusha, Shinyanga, Geita, Mwanza, Simiyu, Tanga, Manyara, Singida, Dodoma na Mara.

Kati ya mbuzi wote waliopo Tanzania, zaidi ya milioni 13 wanapatikana katika mikoa hiyo 10 huku mkoa wa Arusha ukiwa kinara kwa kuwa na mbuzi wengi zaidi Tanzania.