November 24, 2024

Wageni 200 kutoka nchi 60 kushiriki tamasha la utalii Tanzania

Tamasha hilo linajulikana kama “Swahili International Tourism Expo” litafanyika Oktoba 18 hadi 20, 2019 Jijini Dar es Salaam.

  • Tamasha hilo linajulikana kama “Swahili International Tourism Expo” litafanyika Oktoba 18 hadi 20, 2019 Jijini Dar es Salaam.
  • Wageni hao watapata fursa ya kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Dar es Salaam. Wageni zaidi ya 200 kutoka katika nchi 60 duniani wanatarajia kushiriki katika tamasha la utalii hapa nchini litakalofungua fursa mbalimbali kwa Watanzania ikiwemo sekta ya utalii. 

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imesema imejipanga vema kuwapokea wageni wote waliothibitisha kushirikia tamasha hilo lijulikanalo kama Tanzania la “Swahili International Tourism Expo”. 

Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Devotha Mdachi amewaambia wanahabari Jijini Dar es Salaam leo (Agosti 21, 2019),  kuwa tamasha hilo litafanyika  Oktoba 18 hadi 20 mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, 

Amesema mawakala zaidi ya 200 kutoka nchi 60 wanatarajia kushiriki katika maonyesho hayo ambapo kwa kushirikiana na balozi za mbalimbali za nje wamejipanga vema kuwapokea na kuwahudumia kipindi chote watakachokuwepo nchini. 

“Mpaka sasa tumepokea uthibitisho kutoka ofisi za ubalozi; toka nchi mbalimbali zikiwemo Ubalozi wa Sweden, Ubalozi wa Tanzania nchini Malaysia,  Ubalozi wa Tanzania Nchini China, Ubalozi wa Korea ya Kusini na   Ubalozi wa Japani, 

“Ubalozi wa Kanada, Ubalozi wa Afrika Kusini, Ubalozi wa Omani, Ubalozi wa India,  Ubalozi wa Uingereza na Ubalozi wa Brazili,” amesema Mdachi. 


Zinazohusiana:


Aidha, amesema wageni hao watapata fursa ya kutembelea maeneo ya utalii yaliyopo nchini ikiwemo  Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Uduzungwa, Mikumi na   fukwe za Tanga.

Pia watatembelea mapango ya Amboni, Mlima Kilimanjaro, miradi ya Utalii wa Utamaduni mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, pia visiwa vya Zanzibar na Mafia.

Sambamba na hilo, kampuni na mashirika mbalimbali  zaidi ya 30 yamejitolea kuunga mkono juhudi hizo zinazofanywa na TTB katika kuelekea kilele cha Maonyesho hayo.