Wasichana vichwa masomo ya Sayansi kidato cha sita 2019
Kati ya wasichana 10 waliopo kwenye orodha hiyo, wanne wanatoka Shule ya Sekondari ya St Mary’s Mazinde Juu mkoani Tanga.
- Kati ya wasichana 10 waliopo kwenye orodha hiyo, wanne wanatoka Shule ya Sekondari ya St Mary’s Mazinde Juu mkoani Tanga.
Dar es Salaam. Huko waliko wamejawa na furaha. Hawaamini wanachokisikia.
Huenda wakati wanafanya mtihani wa kidato cha sita mwaka huu mabinti hao hawakuwa wanatarajia kuwa wangekuwa vinara katika masomo ya sayansi nchini.
Hata hivyo, matokeo yaliyotangazwa leo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde yamewaweka juu katika masomo ambayo hutazamwa kama ni magumu zaidi kuliko yote na kwa miaka ya nyuma yalikuwa yakitawaliwa na wavulana.
Dk Msonde ameainisha majina 10 bora ya wasichana waliotisha katika masomo ya Sayansi kitaifa wakiongozwa na binti kutoka Shule ya Sekondari ya St Mary’s Mazinde Juu, Faith Matee.
Faith pia ndiye mwanafunzi bora katika Sayansi kitaifa akiwapoteza wavulana katika orodha hiyo ya dhahabu. Msichana mwingine aliyeingia katika orodha hiyo ni Levina Chami kutoka St Mary Goreti iliyopo mkoani Kilimanjaro.
Zinazohusiana:
- Kisimiri sekondari inavyozikimbiza shule kongwe, binafsi Tanzania
- Hizi ndizo shule zinazong’ang’ania mkiani matokeoa kidato cha sita
- Mtwara inavyotikisa matokeo ya kidato cha sita.
Kati ya wasichana hao 10 bora katika masomo ya Sayansi, wanne wanatoka Shule ya St Mary’s Mazinde Juu iliyopo mkoani Tanga huku wawili wakitokea Shule ya Wasichana ya Tabora. Shule ya Wasichana ya Tabora ni shule ya umma huku zote zilizosalia katika orodha hiyo ni za binafsi au mashirika ya kidini.
Hawa ndiyo mabinti waliotisha katika masomo ya Sayansi mtihani wa kidato cha sita mwaka 2019.
1. Faith Nicholaus Matee (PCB) – St Mary’s Mazinde Juu.
2. Levina Calist Chami (PCM) – St Mary Goreti.
3. Wahida A Janguo (PCM) – Feza Girls.
4. Vanessa R Rutabana (PCB) -Tabora Girls.
5. Pielina M Figowole (PCB) – Tabora Girls.
6. Loveness S Mloge (PCB) – St Mary’s Mazinde Juu.
.7. Wahda Mbarak Uzia (PCM) – Zanzibar Feza.
8. Beatrice Martin Mwella(PCM) – St Mary’s Mazinde Juu.
9. Consolata Seraphin Matee (PCB) – St Mary’s Mazinde Juu.
10. Maimuna A Mshana (PCB) – Marian Girls.
Ufaulu huo unawapa fursa wasichana hao kuendelea na masomo ya sayansi na teknolojia katika elimu ya juu ambako huwa kuna wasichana wachache ambao hujikita huko.