November 24, 2024

Kwanini biashara nyingi zinakufa kabla ya kufikisha mwaka mmoja?

Ni kwa sababu waanzilishi hawazingatii nguzo muhimu zinavyohitajika kuisimamisha biashara.

  • Ni kwa sababu waanzilishi hawazingatii nguzo muhimu zinavyohitajika kuisimamisha biashara.
  • Wanajiona wanajua kila kitu, wakati baadhi ya maeneo yanahitaji wataalam.

Kila anayeanzisha biashara hata ikiwa ndogo kiasi gani hupenda kuona inakua na kuimarika ikiwezekana kudumu muda mrefu katika soko la ushindani. 

Lakini matarajio ya wengi huyeyuka hata kabla biashara haijafikisha mwaka mmoja au miaka miwili. Biashara nyingi ndogo ndogo huishia katika kipindi hicho na kushindwa kuendelea mbele. 

Huenda wewe ni mmoja wa watu ambao wamekuwa wakianzisha biashara lakini hazidumu wala kukua katika kiwango unachotaka. Hizi ni miongoni mwa sababu kwanini biashara nyingi ndogo zinakufa kabla ya kufikisha mwaka mmoja:-

Sababu halisi ya wafanyabiashara wengi kushindwa ni kwa sababu hawaelewi mfumo wa biashara ulivyo na jinsi muunganiko wa maeneo muhimu ya biashara unavyofanya kazi. 

Watu wengi wanaoanza biashara wanajiona kuwa wataalam wa kila jambo yaani bidhaa au huduma wanazopanga kuuza. Wanaamini kwamba kile wanachouza ni biashara, kumbe sio!

Mwalimu wa ujasiriamali anayemiliki kampuni ya DIY Business Classes, Steve Chapman kutoka nchini Marekani anaeleza katika moja ya madarasa yake kuwa biashara ni kama gari. Linamchukua mtu toka sehemu moja hadi nyingine. 

Gari linajumuisha sehemu mbalimbali muhimu ambazo kama hazifanyi kazi kwa pamoja haliwezi kutembea. 

Anaeleza kuwa biashara inafanya kazi sawa na gari, ukuaji wake unategemea ushirikiano wa pamoja wa vijenzi vyote vinavyohitajika katika biashara. 

Haya ndiyo maeneo matano muhimu kwa ujenzi wa biashara imara ili ikue na kuendelea mbele kwa muda mrefu.

Watambue mapema watumiaji wa bidhaa yako. Wanapendelea vitu gani na hadhi ipi ili kurahisisha jinsi ya kuwafikia kwa njia mbalimbali.

Lakini biashara ni mtaji na uwekezaji ambao unaweza kuwa wana namna mbalimbali ikiwemo ujuzi, maarifa na hata fedha ili kuipa uhai na iendelea kukua kila siku. 

Kama biashara inakua unahitaji kuwa na mfumo mzuri wa usambazaji bidhaa ili kuhakikisha zinawafikia wateja kwa urahisi bila kuwa na usumbufu wowote wa kutopatikana. Hapa unahitaji kuwa timu nzuri ya watu waliobobea katika usafirishaji na usambazaji wa bidhaa.


 Soma zaidi: 


Ongeza wigo wa masoko na matangazo ya biashara yako. Biashara ni kujitangaza, bidhaa zako hazitafahamika kama hazijulikani na watu. Tengeneza mkakati wa masoko na matangazo ikiwezekana tenga bajeti maalum kwa ajili ya shughuli hiyo. 

Na mwisho wafahamu vizuri washindani wako, itakusaidia kujua mbinu wanazotumia kufanikiwa na kuendelea kuwepo katika soko la bidhaa. 

Hata hivyo, ili ufanikiwe zaidi wekeza katika kujifunza maarifa au njia mpya za kufanya biashara kuendana na mabadiliko katika ulimwengu wa biashara.