October 7, 2024

Mnara wa Eiffel nchini Ufaransa wafungwa kwa muda usiojulikana

Umefungwa jana baada mwanaume mmoja kukutwa akipanda juu ya mnara huo bila ruhusa.

Mnara wa Effeil uliopo Paris, Ufaransa umefungwa kwa muda usiojulikanana. Picha|Mtandao.


  • Umefungwa jana baada mwanaume mmoja kukutwa akipanda juu ya mnara huo bila ruhusa.
  • Watalii waondolewa eneo hilo na washauriwa kusitisha safari za kutembelea mnara huo. 

Mnara wa Eiffel uliopo katika jiji la Paris nchini Ufaransa ambao hutumika kama kituo cha shughuli za utalii umefungwa kwa muda usiojulikana baada ya mwanaume mmoja kukutwa akipanda kuelekea juu ya mnara huo bila ruhusa.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Associated Press, mwanaume huyo alikutwa kiasi cha futi 900 juu ya mnara huo na bado haijajulikana aliwezaje kupenya viunzi vya maafisa wa usalama wanaolinda eneo hilo mpaka kufikia hatua ya kutaka kupanda mpaka juu ya mnara huo. 

Kutokana na kadhia hiyo, watalii takriban 2,500 waliokuwepo katika eneo hilo waliondolewa mara moja na mnara huo umefungwa kwa muda usiojulikana.  Uamuzi wa kuufunga mnara huo ulifikiwa jana (Mei 20, 2019).


Inayohusiana: Haya ndiyo maeneo yanayotembelewa zaidi na watalii duniani


Kampuni inayosimamia mnara huo ya The Eiffel Tower Exploitation Company imewashauri watalii wanaokusudia kutembelea eneo hilo siku za hivi karibuni kusitisha safari zao mpaka pale watakapopewa taarifa. 

Si mara ya kwanza kwa watu kujaribu kupanda hadi katika kilele cha mnara wa Eiffel. Mwaka 2015, mkimbiaji huru wa Uingereza, James Kingston alipanda bila kamba za usalama wala ruhusa. 

Mnara huo ni mrefu zaidi nchini Ufaransa ukiwa na mita 324 ikiwa ni sawa na jengo la ghorofa 81.