November 24, 2024

Fursa za ajira ujenzi wa kiwanda cha upigaji rangi bomba la mafuta Tabora

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda hicho cha upigaji rangi mabomba ya mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoimo nchini Uganda hadi Tanga kutafungua fursa za kibiashara na ajira hasa kwa wananchi wa mikoa ya Tab

Ujenzi wa bomba lenye urefu wa kilometa 1,410 ambalo litasafirisha mafuta ghafi kutoka ziwa Albert nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga. Utarajiwa kuzalisha ajira za moja kwa moja 1,500 na ajira zisizo za moja kwa moja 20,000. Picha|Mtandao.


  • Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda hicho cha upigaji rangi mabomba ya mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoimo nchini Uganda hadi Tanga kutafungua fursa za kibiashara na ajira hasa kwa wananchi wa mikoa ya Tabora na Shinyanga.
  • Mkandarasi anatarajiwa kukabidhiwa eneo la mradi na kupeleka vifaa Septemba 2019. 

Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda cha upigaji rangi mabomba ya mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoimo nchini Uganda hadi Tanga kutafungua fursa za kibiashara na ajira hasa kwa wananchi wa mikoa ya Tabora na Shinyanga.

Kiwanda hicho kinatarajiwa kujengwa katika kijiji cha Sojo kata ya Igusule wilaya ya Nzega mkoani Tabora karibu na eneo la reli inayoenda Isaka mkoani Shinyanga ambako zitajengwa ofisi za mradi huo. 

Mgalu aliyekuwa akizungumza bungeni leo (April 10, 2019) amesema tafiti mbalimbali zimeendelea kufanyika kuhusisha ujenzi wa miundombinu ikiwemo reli na ofisi mbalimbali za mradi wa kiwanda hicho katika eneo la Isaka ili kufungua fursa za kiuchumi na kijamii. 

Amesema Igusule na Isaka siyo mbali, hivyo itatoa fursa za ajira na biashara kwa wananchi wa maeneo hayo mradi utakapoanza kujengwa. 

“Eneo la Igusule ni kama kilomita tano kutoka Isaka, kwa hiyo ni wazi kabisa wananchi wa maeneo ya Isaka na maeneo mengine ya mkoa wa Shinyanga na Tabora watapata fursa mahususi kabisa katika mradi huu ikiwemo ajira na masuala mengine ya kibiashara,” amesema Mgalu.

Mgalu ametoa maelezo hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige aliyetaka kujua ni maandalizi gani ya jumla yamefanyika kwa ajili ya kuwaandaa wananchi  wa Isaka na Igusule ili waweze kushiriki katika mradii huo ikiwemo kufaidika na fursa za ajira na biashara. 


Zinazohusiana: 


Ujenzi wa kiwanda hicho muhimu katika mradi wa bomba utaanza tu mara baada ya kukamilika kwa zoezi la kuthaminisha na kutoa ardhi husika na kukabidhiwa wakandarasi wa ujenzi. 

Kwa sasa taratibu za utoaji ardhi ziko katika hatua za mwisho na zinatarajiwa kukamilika mapema Julai, 2019. Mkandarasi anatarajiwa kukabidhiwa eneo la mradi na kupeleka vifaa Septemba 2019. 

“Aidha mpango wa usimamizi wa mazingira na jamii umekamilika na kuidhinishwa na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC),” amesema.

Ujenzi wa bomba lenye urefu wa kilometa 1,410 ambalo litasafirisha mafuta ghafi kutoka ziwa Albert nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga. Utarajiwa kuzalisha ajira za moja kwa moja 1,500 na ajira zisizo za moja kwa moja 20,000.