November 24, 2024

Afrika haitafaidika na kupungua kwa gharama za uagizaji chakula 2019

Ripoti mpya ya makadirio ya chakula ya shirika la chakula duniani (FAO) imesema gharama ya uagizaji wa chakula duniani kwa mwaka 2019 zitapungua kutokana na ongezeko la uzalishaji wa bidhaa lakini nchi za Afrika hazitanufaika.

Ripoti hiyo ambayo ni muhimu kwa shughuli za uchumi duniani imejikita kufanya tathmini ya soko na mwenendo wa uzalishaji wa bidhaa muhimu hasa nafaka, samaki, sukari, mafuta ya kula, maziwa na nyama. Picha|Mtandao.


  • Ripoti mpya ya makadirio ya chakula ya shirika la chakula duniani (FAO) imesema gharama ya uagizaji wa chakula duniani kwa mwaka 2019 zitapungua kutokana na ongezeko la uzalishaji wa bidhaa lakini nchi za Afrika hazitanufaika.
  • Lakini itakuwa ni shangwe kwa nchi maskini kwa sababu bei ya mafuta yatokanayo na mboga inatarajiwa kupungua.

Dar es Salaam. Ripoti mpya ya makadirio ya chakula iliyotolewa na shirika la chakula duniani (FAO) imesema gharama ya uagizaji wa chakula duniani kwa mwaka huu wa 2019 zitapungua kutokana na ongezeko la uzalishaji wa bidhaa lakini nchi za Afrika hazitanufaika na punguzo hilo.

Ripoti hiyo ambayo imetolewa jana (Mei 9, 2019) katika jiji la Rome, Italia imeeleza kuwa gharama za uagizaji wa chakula zitapungua kwa dola za Marekani 1.4  trilioni ambazo ni sawa na asilimia 2.5 ikiliganishwa na mwaka uliotangulia.

Wanufaika wa kupungua kwa gharama hizo ni nchi zilizoendele wakati kwa nchi za Afrika hasa  za  Kusini mwa Jangwa la Sahara gharama inatarajiwa kuongezeka.

Kwa mujibu wa taarifa ya FAO iliyochambua ripoti hiyo imeeleza kuwa kwa kupungua kwa gharama kunaweza kusababisha chakula kingi zaidi  kuagizwa na kupunguza thamani ya sarafu dhidi ya dola ya Marekani ambayo inatumika katika miamala ya kimataifa katika nchi zinazoendelea.

“Gharama za uagizaji kahawa, chai, kakao na viungo inakadiriwa kupungua kwa karibu asilimia 50 lakini gharama ya kuagiza sukari na nafaka itasalia kama ilivyo,” imesema ripoti hiyo ambayo hutolewa mara mbili kwa mwaka. 


Zinazohusiana:


Lakini itakuwa ni shangwe kwa nchi maskini kwa sababu bei ya mafuta yatokanayo na mboga ambayo yanaagizwa zaidi na nchi inatarajiwa kupungua na hivyo kuwaletea ahueni ya maisha wananchi wa maeneo husika ikiwemo Tanzania. 

Inakadiriwa kuwa Tanzania inaagiza tani zisizopungua 400,000 za mafuta ya mawese kila mwaka hasa kutoka Malaysia ili kufidia pengo la uhaba wa mafuta, licha ya uwezo wa uzalishaji wa mbegu zingine za mafuta. 

Ripoti hiyo ambayo ni muhimu kwa shughuli za uchumi duniani imejikita kufanya tathmini ya soko na mwenendo wa uzalishaji wa bidhaa muhimu hasa nafaka, samaki, sukari, mafuta ya kula, maziwa na nyama.