Ubabe wa Pemba katika uzalishaji wa karafuu
Asilimia 94 ya uzalishaji wa karafuu visiwani Zanzibar ulirekodiwa katika mikoa ya Kusini Pemba na Kaskazini Pemba.
- Asilimia 94 ya uzalishaji wa karafuu visiwani Zanzibar ulirekodiwa katika mikoa ya Kusini Pemba na Kaskazini Pemba.
- Karafuu ni zao kuu la biashara visiwani Zanzibar na sehemu kubwa ya wakulima hunufaika kutokana na kujikita na uzalishaji wake.
Dar es Salaam. Unaweza sasa kusema kuwa Pemba ndiyo kitovu cha uzalishaji karafuu nchini baada Ripoti ya utafiti wa mwaka wa kilimo kwa mazao na mifugo mwaka 2016/17 ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu kubainisha kuwa asilimia 94.1 ya uzalishaji wa zao visiwani Zanzibar ulitoka katika mikoa ya Kusini Pemba na Kaskazini Pemba.
Karafuu ni moja ya mazao yanayochangia kuingiza fedha za kigeni nchini hususan visiwani Zanzibar sanjari na korosho, chai, kahawa na mkonge.
Katika mwaka unaoishia Januari 2019 takwimu za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zinaonyesha kuwa karafuu Dola za Marekani 8.6 milioni (Sh19.8 bilioni) kutoka Dola za Marekani 54.2 milioni (Sh124.7 bilioni) kipindi kama hicho mwaka jana kutokana na mwenendo wa msimu wa uzalishaji wa zao hilo.
Zao hilo ambalo hutumika kama kiungo lina faida lukuki kwa binadamu zikiwemo kuongeza kinga za mwili, kuongeza mmeng’enyo wa chakula na kulinda ini.
Visiwani Zanzibar, karafuu ni zao kuu la biashara na sehemu kubwa ya jamii ya wakulima hunufaika kutokana na kujikita kulizalisha.
Hata hivyo, kikubwa ambacho hakifahamiki zaidi ni jekiasi ganicha zao hilo huzalishwa Tanzania Bara. Je, maeneo hayo ya Tanzania Bara yanazalisha kiwango gani cha karafuu?