November 24, 2024

Wajua vipaumbele vya Watanzania wanapopata Pesa?

Kwa mujibu wa Utafiti wa hali ya huduma za kifedha Tanzania ujulikanao kama Finscope uliofanyika mwezi wa Aprili na Julai mwaka 2017, ukiachana na chakula na mavazi Watanzania hutumia zaidi fedha zao kwenye huduma za afya kwa asilimia 11 na kufuatiwa na e

Dar es Salaam. Umeshawahi kujiuliza Watanzania hutumia fedha wapi ukiachilia matumizi ya lazima ya chakula na mavazi?

Kwa mujibu wa Utafiti wa hali ya huduma za kifedha Tanzania wa Finscope  uliofanyika mwezi wa Aprili na Julai mwaka 2017 Watanzania hutumia zaidi fedha zao kwenye huduma za afya kwa asilimia 11 na kufuatiwa  na elimu kwa asilimia 10.

Utafiti  huo  pia unaonyesha kuwa vipaumbele vikubwa katika miji kama Dar es Salaam na mingine ni kodi za nyumba ikifuatiwa na elimu.