November 25, 2024

Fahamu visiwa viwili vinavyoongoza kwa ukubwa Tanzania bara

Ni visiwa cha Ukerewe kilichopo katika Ziwa Victoria pamoja na kisiwa cha Mafia katika bahari ya Hindi.

  • Ni visiwa cha Ukerewe kilichopo katika ziwa Victoria pamoja na kisiwa cha Mafia katika bahari ya Hindi.
  • Visiwa hivyo vimezungukwa na vivutio mbalimbali vya utalii ambavyo vikitumika vizuri vitasaidia kukuza sekta ya utalii nchini.

Dar es Salaam. Tanzania ni nchi iliyobarikiwa kuwa na vivutio vingi katika bahari hadi nchi kavu ambavyo vinazidi kuipa thamani nchi hasa kwenye sekta ya Utalii.

Hata hivyo moja ya sehemu zinazovutia watu zaidi ni visiwani ambapo watu wanapata nafasi ya kuvuka maji na kwenda kujionea mandhari ya kuvutia hasa fukwe.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Taifa ya Takwimu za Mazingira mwaka 2017-Tanzania Bara inaonyesha visiwa vikubwa viwili ambavyo ni Kisiwa cha Ukerewe chenye kilometa za mraba 647 kilichopo Katika Ziwa Victoria.

Huku cha pili ni kisiwa cha Mafia kilichopo katika Bahari ya Hindi chenye Kilomita za mraba 518. Visiwa hivi ni asilimia 0.12 ya ardhi iliyopo nchini Tanzania.

Maeneo haya yote yamebarikiwa kuwa na hali ya hewa nzuri na vivutio mbalimbali vya utalii vinavyofanya watalii kwenda kujionea kama vile fukwe, mazingira na maeneo mbalimbali ya historia.