TMA yatahadharisha ujio wa mvua kubwa
Mvua hizo zinaweza kusababisa mafuriko katika mitaa na foleni kali maeneo ya mjini.
- Mvua hiyo itakuwa katika mkoa ya Dar es Salaam, Pwani na Tanga pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba.
- Mvua hizo zinaweza kusababisa mafuriko katika mitaa na foleni kali maeneo ya mjini.
Dar es salaam. Ndani ya siku tatu zijazo huenda hali ya Jiji la Dar es Salaam ikabadilika ghafla baada ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kutahadharisha kutokea kwa mvua kubwa kuanzia Septemba 26 hadi Septemba 27, 2018.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na TMA leo jioni (Septemba 25,2018) imetaja mikoa itakayoathirika na mvua hiyo ni baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es salaam, Tanga na Pwani pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Utabiri huo kutoka TMA umewataka wananchi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari kwa sababu mvua hizo.
Utabiri wa Hali ya Hewa wa siku tano na athari zinazoweza kutokea. Umetolewa leo tarehe 25/08/2018 na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania @tma_services
#utabiriTZ
#5daysforecast
pic.twitter.com/kGgKmcofJs— Tanzania Met Agency (@tma_services) September 25, 2018
Yanayokuhusu: Watanzania washauriwa kutumia taarifa za hali ya hewa kwenye mipango ya maendeleo
Ujio mfumo wa taifa wa hali ya hewa kuchochea ujenzi wa viwanda nchini
Usafiri, biashara kuwa sehemu ya mwelekeo hali ya hewa Dar
TMA imeeleza madhara yanayoweza kutokana na mvuo hizo kwa wananchi na mali zao.
“Madhara yatakayotokana na mvua hiyo ni kutokea mafuriko katika mitaa na kusababisa msongamano wa magari na watu hivyo kuchelewasha usafirishaji hasa katika maeneo ya mjini,’’ imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.