Kobe mwenye vichwa viwili atimiza miaka 20
Maajabu katika hii dunia hayajawi kuisha septemba 3 kobe aitweye star Janus amesherekea miaka 20 toka kuzaliwa kwake.
Kobe huyo mwenye vichwa viwili ambaye anatuzwa huko katika jumba la makumbusho la kihistoria la Geneva (Geneva Museum of Natural History’s) akiwa kobe mwenye maumbile ya kipekee kabisa.
Jina hilo la Janus ambalo kobe huyo amepewa linatokana na jina la miungu ya kirumi Janus .Janus (star janus) alizaliwa spetemba 3 1997, katika jumba la Makumbusho la kihistoria la Geneva kutoka katika yai lilokuwa kwenye atamizi.
Watafiti wanasema wanyama wenye vichwa viwili ni nadra kuishi muda mrefu ,lakini jumba la Makumbusho la kihistoria la Geneva limefanya kazi kubwa na yaziada mpaka kufanikisha rekodi hiyo ya manyama mwenye maumbile kama hayo kuishi muda mrefu.
Kobe huyo ambae anaishi vizuri kwenye makumbusho hayo ndio anae shikilia rekodi ya kobe wenye vichwa viwili aliyeishi kwa muda mrefu mpaka sasa.