Tanzania yaanza mazungumzo na wawekezaji bandari ya Bagamoyo
Rais Samia Suluhu Hassan aeleza kuwa Serikali imeanza mazungumzo na wawekezaji wa mradi huo ili uendelee na kuleta faida kwa taifa.
Rais Samia Suluhu Hassan aeleza kuwa Serikali imeanza mazungumzo na wawekezaji wa mradi huo ili uendelee na kuleta faida kwa taifa.
Rais Samia Suluhu Hassan amesema tayari kuna wagonjwa wa Corona ambao wameshaonekana nchini katika wimbi la tatu huku akiwataka viongozi wa dini kupaza sauti kwa waumini wao na Watanzania wachukue tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo.
Ni soko maarufu katika Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita ambalo ni kiungo muhimu cha biashara ya bidhaa mbalimbali za nyumbani.
Ndani ya mwaka mmoja deni hilo limeongezeka kwa zaidi ya Sh5 trilioni kutokana na uwekezaji katika miradi ya maendeleo.
Tanzania na Burundi bado hazijaanza kutoa chanjo dhidi ya Corona kwa raia wake.
Licha ya Serikali kuruhusu usafirishaji wa makinikia (mchanga wa madini), imesema makinikia yote yanayosafirishwa nje ya nchi yamefuata utaratibu na hakuna yanayouzwa bila kulipiwa kwanza.
Mradi huo wa kusindika gesi asilia na kuwa kimiminika (LNG) utakaojengwa mkoani Lindi unatarajiwa kuanza Julai, 2023 ukipigwa kalenda ya mwaka mmoja zaidi ya mipango ya awali.
Ni Misrah na wahamiaji wengine 55 waliopata dhuruba ndani ya mashua iliyomilikiwa na wasafirishaji waliokuwa wakivuka Ghuba ya Aden kuingia nchini Yemen kutoka Pembe ya Afrika kupitia Djibouti, Aprili 14 mwaka huu.
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeanza kufanya maboresho ya huduma za uwekezaji kwa kuunganisha mifumo ya kielektroniki kwa taasisi na idara 11 za Serikali zinazotoa huduma kwenye kituo cha pamoja cha uwekezaji.
Serikali ya Tanzania na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) zimesaini mikataba miwili ya mkopo wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 140 (takriban Sh323.4 bilioni) kwa ajili ya kufadhili mradi wa kufua umeme wa nguvu ya maji wa Malagarasi uliopo mkoan
Ni filamu ya “Those Who Wish Me Dead” inamuhusu Conor, kijana mwenye umri wa miaka 12 anayepambana ili kufikia ya ndoto ya baba yake.
Wakati Tanzania ikishauriwa kuanza kutoa chanjo ya Corona kwa raia wake, Waziri wa Afya wa Ujerumani Jens Spahn amesema nchi yake itaanza kutoa chanjo hiyo kwa kila mtu kuanzia Juni 7 mwaka huu.
Amelitaka Jeshi la Polisi Tanzania kutumia sheria na adhabu kudhibiti uhalifu kuliko kuzitumia kama kitega uchumi cha kujipatia mapato yotokanayo na faini na tozo za makosa yakiwemo ya usalama barabarani.
Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko makubwa ya wakuu wa mikoa Tanzania Bara huku baadhi wakibadilishiwa vituo, wakiondolewa na kuingiza wapya akiwemo David Kafulila ambaye anakua Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Sylvester Mwakitalu kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP). Mwakitalu anachukua nafasi iliyoachwa na Biswalo Mganga ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Mikoa 11 ukiwemo Mkoa wa Tanga haijaweza kufikia wastani wa kitaifa wa upatikanaji wa dawa kimkoa, jambo linaloweka afya za Watanzania mashakani kwa kukosa matibabu kwa wakati.
Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa (UN) imeeleza kuwa madhara ambayo dunia imeyapata hasa ya kiuchumi yaliyotokana na janga la virusi vya corona yangeweza kuzuilika iwapo Serikali za nchi zingechukua hatua za haraka.
Serikali ya China imeipatia Tanzania msaada wa Yuan za China milioni 100 sawa na Sh35.4 bilioni utakaotumika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwa ni moja ya hatua inayolifanya taifa hilo la Asia kuendeleza mizizi ya urafiki na Tanzania.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima amesema wizara yake inakusudia kuwasilisha muswada wa Sheria ya Bima ya afya kwa Wote bungeni Juni mwaka huu.
Ameziagiza taasisi na mamlaka ambazo zinashiriki kuendeleza wabunifu nchini Tanzania zihakikishe zinawawezesha wabunifu wanaochipukia kuziendesha kazi zao za ubunifu na uvumbuzi kibiashara.