LIVE: Rais Samia Suluhu Hassan anahutubia Bunge la Tanzania
Rais Samia Suluhu Hassan analihutubia Bunge jijini Dodoma kwa mara ya kwanza tangu aapishwe Machi 19, 2021.
Rais Samia Suluhu Hassan analihutubia Bunge jijini Dodoma kwa mara ya kwanza tangu aapishwe Machi 19, 2021.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewataka watumiaji wa bahari ya Hindi katika mikoa ya Lindi na Mtwara kuchukua tahadhari kutokana kuwepo kwa kimbunga Jobo kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar ambacho kinaweza kusababisha ongezeko la upepo na mawimbi
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imebaini kuwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) lilipata hasara ya Sh60 bilioni katika mwaka wa fedha wa 2019/20 lakini mapato na matumizi ya shirika hilo yamekuwa yakiongezeka.
Umesheheni mandhari nzuri na yenye kuvutia kwa watalii wa ndani na unapatikana Wilayani Muheza Mkoa wa Tanga.
Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2019/20 imeibua ubadhirifu mkubwa wa matumizi ya fedha katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ukiwemo upotevu wa zaidi ya Sh3 bilioni.
Ni Mkurugenzi wa Fedha wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Suzana Chaula baada ya kutoridhishwa na utendaji wake ikiwemo kutokutumia mashine za kielektroniki kukata tiketi.
Faida kabla ya kodi ya benki hiyo imeongezeka kwa Sh61 bilioni sawa na asilimia 35 ndani ya mwaka mmoja licha ya mwaka 2020 kuwa na changamoto ya maradhi ya Corona
Ni kati ya 2,400 waliokuwa wameahidiwa ajira jeshini na Hayati Rais Magufuli baada ya kushiriki katika ujenzi wa Ikulu ya Chamwino, Dodoma.
Mambo muhimu yaliyoibuliwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu matumizi ya fedha za umma katika taasisi za umma katika namba.
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amewataka Wabunge wanaotumia usafiri wa bodaboda kuingia na kutoka bungeni kuwa makini na madereva wanaowaendesha ili kulinda usalama wao.
Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya Watu (UNFPA) imeeleza kuwa takribani nusu ya wanawake wote katika nchi zinazoendelea duniani wananyimwa haki ya kuamua kuhusu miili yao ikiwemo tendo la ndoa, uzazi wa mpango au kutafuta huduma za afya
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema katika bajeti ya mwaka 2021/22 wizara yake itaweka mikakati mbalimbali ya kukuza na kuimarisha sekta ya umwagiliaji ikiwemo kubadilisha mfumo wa utendaji wa Tume ya Umwagiliaji (NIC) ili kuondokana na matatizo
Mtarajio ya wafanyakazi ni kuona anatoa mwelekeo mpya wa utatuzi wa changamoto zao za muda mrefu ikiwemo nyongeza ya mishahara.
Ni pamoja na kunawa mikono kabla ya kuandaa chakula na baada ya kukutana na watu mbalimbali.
Walimu na wanafunzi waelimishwe kwa uwazi kuhusu dalili na kinga ya COVID-19. Pia umuhimu wa kunawa mikono, kuvaa barakoa na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Damas Ndumbaro amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devota Mdachi kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu zinazomkabili.
Abaini uwepo wa kadi 426,757 zenye thamani ya Sh3.4 bilioni ambazo zimeharibika na hazifai kwa matumizi na matumizi yasiyo sahihi ya taarifa za watu waliosajiliwa kwenye kanzidata ya NIDA.
Kabla ya kupata chanjo utapewa ushauri na mto huduma za afya kama unastahili kupata chanjo au la!
Bei ya petroli na dizeli imepanda kwa miezi miwili mfululizo nchini Tanzania, jambo linalowafanya wamiliki wa vyombo vya moto kutoboa zaidi mifuko yao ili kuipata nishati hiyo muhimu katika ukuaji wa shughuli za kiuchumi.
Hadi jana Aprili 7 watu zaidi ya 200,000 katika nchi za Afrika Mashariki walikuwa wameambukizwa ugonjwa wa Corona huku 3,067 kati yao wakifariki dunia.