Wachambuzi wa biashara waelezea Jumia kufunga vilago Tanzania
Hatua hiyo ya Jumia inakuja siku chache baada ya kusimamisha oparesheni zake nchini Cameroon kusema inaangazia masoko sehemu nyingine duniani.
Hatua hiyo ya Jumia inakuja siku chache baada ya kusimamisha oparesheni zake nchini Cameroon kusema inaangazia masoko sehemu nyingine duniani.
Wapo watu wanaacha taa zikiwaka mchana kutwa ama kusahau kuzima feni na televisheni na usahaulifu mwingine huku wakisahau ukweli wa kwamba sababu za matumizi makubwa ya umeme ni nyingi na zinasababishwa na makosa ya kila siku.
Black Friday ni muda maalumu ambapo maduka hufunguliwa wakati wa jioni na bidhaa huuzwa kwa bei ya chini mno kuliko mteja anavyotarajia na watu hutumia siku hiyokununua bidhaa kwa ajili ya maandalizi ya zawadi za Krismas na kufunga mwaka.
Vipi kama ukiweka tai na umaridadi wako pembeni na kuvalia viwalo vya kawaida ili utimbe ndani ya kumbi za sinema kwaajili ya burudani yako ya wikiendi?
Kwanini yaongelewe ya kale? Mbali na kuwa na skrini mbili, hizi ndizo sababu nyingine za Razr 2019 inayotumia mfumo endeshi wa Android kuuzwa zaidi ya Sh3.45 milioni.
Maswali ya “pesa nitatoa wapi”, “je nitafanikiwa”, “vipi ikinyesha mvua” yanaweza kuwa ni kati ya maswali machache yanayo zunguka akilini mwako.
Mfumo huo unao kadiriwa kuokoa wastani wa shilling bilioni 34 katika miaka mitano ya kwanza umetayarishwa kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2011 na Kanuni za Ununuzi wa Umma chini ya Tangazo la Serikali Na. 446 la Mwaka 2013.
Kitendo cha mtandao huo kutoruhusu matangazo ya kisiasa kimekuja na lengo la kuwafanya wanasiasa kufanya kazi ili kutumia ushawishi wao na siyo kununua ushawishi wao kwa njia ya matangazo ambayo yalikuwa yakiruhusiwa kwenye mandao huo.
Programu hizo zinasababisa betri ya simu kuisha kwa uharaka na zaidi, zinachochea matumizi makubwa ya intaneti huku zingine zikichukua taarifa binafsi za mtumiaji.
Azam ambayo imeingiza sokoni programu tumishi (App) hiyo ya Sarafu ambayo inamuwezesha mtu kununua bidhaa siyo tuu za azam bali na zingine muhimu kama sabuni, sukari, mafuta na mengineyo na kufanya kurahisisha manunuzi ya jumla.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo imeahirisha kutangaza mwenendo wa mfumuko wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka unaoishia Oktoba 2019 kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake, badala yake itatangaza jumatatu ya Novemba 11.
“Doctor Sleep” na “Midway”; filamu hizi zilizoingia sokoni hivi karibuni, zina visa vingi vya kufikirika lakini vyenye uhalisia wa maisha, zitaonyeshwa kwa wiki nzima kuanzia leo (Novemba 8, 2019) katika kumbi mbalimbali za sinema.
Soma maelezo kabla ya kupakua programu kwenye simu yako na pendelea kutumia apps zilizopo kwenye duka la programu za simu linalotambulika.
Licha ya kwamba Serikali imelipa Sh417 bilioni kwa wakulima wa pamba, bado baadhi ya wakulima hawajalipwa pesa zao katika msimu wa mwaka 2018/2019, jambo linalowaletea changamoto ya kushiriki kikamilifu katika kilimo cha zao hilo.
Kati ya teknolojia ambazo zimetengenezwa kurahisisha maisha ya watu ni pamoja na programu tumishi (Apps) za kupanga bajeti binafsi au taasisi kwa ajili ya matumizi sahihi ya mapato na kufikia malengo husika.
Amefariki akiwa na umri wa miaka 73 mwaka huu, lakini historia yake kwenye ulimwengu wa mapishi haitafutika kirahisi katika mioyo ya watu wasiojiweza duniani.
Huenda unajiuliza ni kwanini kila uonapo kompyuta za kisasa, hauoni sehemu za kuweka CD wala DVD na unajiuliza nini kipya kitakuja baada ya teknolojia hiyo kutoweka kabisa. Kwa nini teknolojia hiyo inatoweka kwa kasi?Na nini mbadala wake?
Baada ya Rambo kutamba na “Last blood” huenda visu, mabomu na mitego yake ikasahaulika kwani Anold Schwarzenegger, amerudi kwa kasi.
Mr Beast ambaye alianza safari hiyo Oktoba 25, 2019, alifanikiwa kupanda miti 300 kwa siku moja akishirikiana na marafiki zake wasiopungua 10.
Kutembelea vivutio vilivyopo katika hifadhi hizo ni njia mojawapo ya kuendeleza sekta ya utalii ili kuongeza pato la Taifa na utolewaji wa huduma za kijamii.