July 8, 2024

Bei ya mahindi yashuka Dodoma

Bei ya jumla ya mahindi katika Mkoa wa Dodoma imeshuka kwa takriban asilimia 23.7 ndani ya kipindi cha wiki moja, jambo linawapa ahueni wanunuzi wa zao hilo katika mkoa huo uliopo katikati mwa Tanzania.

  • Bei ya juu ya zao hilo kwa kilo 100 mkoani humo imeshuka hadi Sh45,000 kutoka Sh59,000 Ijumaa iliyopita.
  • Lindi ndiyo mkoa ambao mahindi leo yanauzwa kwa bei ya juu zaidi Tanzania.

Dar es Salaam. Bei ya jumla ya mahindi katika Mkoa wa Dodoma imeshuka kwa takriban asilimia 23.7 ndani ya kipindi cha wiki moja, jambo linawapa ahueni wanunuzi wa zao hilo katika mkoa huo uliopo katikati mwa Tanzania. 

Takwimu za mazao makuu ya chakula zilizotolewa leo (Mei 22, 2020) na Wizara ya Viwanda na Biashara zinaonyesha kuwa bei ya juu ya gunia la kilo 100 la zao hilo linauzwa kwa Sh45,000 katika soko la Majengo mkoani humo.

Hata hivyo, bei hiyo ya juu imeshuka kwa asilimia 23.7 kutoka Sh59,000 iliyorekodiwa Ijumaa Mei 15, 2020 mkoani humo katika soko hilo hilo. 

Katika takwimu za leo, bei ya chini ya zao hilo katika soko hilo la Majengo imeporomoka hadi Sh40,000 kutoka Sh48,000 iliyorekodiwa wiki iliyopita.    

Kushuka kwa bei hiyo ya juu kutawanufaisha zaidi wanunuzi huku wafanyabiashara na wakulima wakipoteza wastani wa Sh14,000 kwa kila gunia moja iwapo hesabu hizo zitapigwa kwa viwango vya bei ya juu. 

 Aidha, takwimu hizo zinaonyesha kuwa bei ya juu ya zao hilo la chakula inayotumika leo ni Sh115,000 katika Mkoa wa Lindi huku bei ya chini ikiwa ni Sh32,000 katika Mkoa wa Ruvuma. 

Endelea kusoma www.nukta.co.tz kwa kwa habari zaidi za takwimu kuhusu bei za mazao, soko la hisa na nyingine za biashara. Kwa habari zaidi Whatsapp +255 677 088 088 au newsroom@nukta.co.tz