Prof Kabudi: Hatutafunga mipaka ya Tanzania
Serikali ya Tanzania imesema itaendelea kuacha wazi mipaka yake licha ya tishio la janga la Corona ili kuruhusu bidhaa muhimu kufika katika nchi zisizo na bandari.
Serikali ya Tanzania imesema itaendelea kuacha wazi mipaka yake licha ya tishio la janga la Corona ili kuruhusu bidhaa muhimu kufika katika nchi zisizo na bandari.
Wakulima na wafanyabiashara huenda ni miongoni mwa watu walionufaika zaidi na zao la mahindi baada ya ripoti mpya kuonyesha kuwa bei ya jumla ya zao hilo ilipanda kwa asilimia 21.5 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Bunge la Tanzania limeidhinisha Sh229.8 bilioni kwa ajili ya bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa fedha wa 2020/21 ambayo inakusudia kutekeleza vipaumbele 10 ikiwemo kuzalisha mbegu bora kwa ajili ya wakulima wa Tanzania.
Miongoni mwa ahueni hizo ni kuruhusu benki na taasisi za fedha kujadiliana na wakopaji juu ya namna ya urejeshaji bora ya mikopo itakayopunguza maumivu.
Mchele ni miongoni mwa mazao makuu ya chakula yanayotegemewa na Watanzania kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo chakula.
Idadi ya vituo vya mafuta ya magari Tanzania Bara imeongezeka kwa asilimia 10 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, jambo linaloongeza ushindani kwa wafanyabiashara na kuwafaidisha zaidi wanunuzi.
Wakazi wa Mkoa wa Lindi leo Mei 8, 2020 wananunua gunia la kilo 100 la viazi mviringo takriban mara tatu ya wenzao wa Mkoa wa Rukwa, jambo linalowafaidisha zaidi wafanyabiashara na wakulima wa zao hilo.
Kasi ya mfumuko wa bei za bidhaa na huduma nchini Tanzania imeshuka hadi kufikia asilimia 3.3 kwa mwaka ulioishia Aprili 2020 kutoka asilimia 3.4 iliyorekodiwa Machi mwaka huu,
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amesema hadi kufikia mwezi Machi 2020 wizara yake haikupata fedha zozote kwa ajili ya shughuli za maendeleo zilizotengwa katika bajeti ya mwaka huu wa fedha wa 2019/2020.
Ahueni hiyo inakuja baada ya EWURA kueleza kushuka kwa bei za nishati hiyo kwa bei za rejareja na jumla kuanzia kesho (Mei 6, 2020) kwa mafuta yanayopitia Bandari ya Dar es Salaam.
Bei ya juu ya gunia la kilo 100 la zao hilo jijini humo ni Sh280,000 katika soko la Tandika kutoka Sh270,000 iliyorekodiwa wiki iliyopita.
Serikali imesema inafanya tathmini ya hali ya ununuzi wa zao la pamba kwa msimu wa mwaka 2019 ili kuondoa changamoto zilizojitokeza kabla msimu mpya wa ununuzi wa zao kuanza mwaka huu ikiwemo kulipa madeni ya wakulima.
Wakati ardhi na nyumba vikiwa rasilimali muhimu kwa ajili ya makazi na shughuli za maendeleo, imebainika kuwa zaidi ya nusu ya Watanzania wanapenda kumiliki rasilimali hizo lakini hawana uwezo wa kuzipata kutokana na changamoto za kipato.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya amewataka wananchi wa Mkoa wa Simiyu kuongeza kasi ya uzalishaji wa zao la pamba sambamba na mazao mengine ya biashara ili kuwa na uhakika wa mapato.
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umetakiwa kubuni njia muafaka ya kuongeza mapato kwa kuhifadhi nafaka zaidi na kufanya biashara ya mazao ya kilimo.
Huenda mkakati wa Serikali kufufua zao la mkonge ukatumia muda mrefu kukamilika, baada ya uzalishaji wa mbegu bora kutoendana na mahitaji ya wakulima ambao wanawekeza katika zao hilo la biashara.
Mmoja aliyesaka ajira bila mafanikio aweka kibindoni Sh4 milioni kwa miezi minne
Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021 imeshuka kwa asilimia 2.4 hadi kufikia Sh899.2 bilioni, ikishuka kwa mara ya pili mfululizo tangu ilivyoanza mwaka 2019/20.
Bajeti ya wizara hiyo ya mwaka 2021/2021 imeongezeka hadi Sh40.2 bilioni kutoka Sh30.8 bilioni mwaka huu.
Gunia la kilo 100 la viazi mviringo katika masoko ya Mtwara linauzwa kwa Sh120,000, wakati masoko ya Rukwa linauzwa kwa Sh45,000.