Bajeti ya Wizara ya Ulinzi yapaa kwa mara ya pili mfululizo
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa inakusudia kutumia bajeti ya Sh2.14 trilioni katika mwaka wa fedha 2020/21 ikiongezeka kutoka Sh1.85 trilioni iliyopitishwa mwaka 2019/20.
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa inakusudia kutumia bajeti ya Sh2.14 trilioni katika mwaka wa fedha 2020/21 ikiongezeka kutoka Sh1.85 trilioni iliyopitishwa mwaka 2019/20.
Ujenzi wa sanamu hiyo unaoratibiwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, tayari upo kwenye hatua za awali na unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba 2020.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) limeeleza kuwa linaangalia uwezekano wa kufungua shule katika nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika ambako wanafunzi wengi hawapati fursa ya kusoma kutokana na janga la Corona.
Kampuni ya habari na teknolojia ya Nukta Africa imeandaa programu maalum ya uthibitishaji taarifa (Fact checking) ambayo itaisaidia jamii kukabiliana na taarifa za uzushi kuhusu CIVID-19 ikiwa ni safari ya kuwa kurasa maalum za kuthibitisha habari kwenye t
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imeliomba Bunge kuidhinisha Sh4.78 trilioni kwa ajili ya bajeti yake ya mwaka 2020/2021 ambayo theluthi mbili ya fedha hizo zimeelekezwa katika sekta ya uchukuzi.
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameelekeza kusimamishwa kazi mara moja kwa Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, Dk Nyambura Moremi na Meneja Udhibiti wa Ubora, Jacob Lusekelo kupisha uchunguzi.
Rais Magufuli ameteua Dk Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk Augustine Mahiga aliyefariki Mei Mosi 2020.
Rais Magufuli katika taarifa yake iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, amesema marehemu amefikishwa hospitali leo (Mei 1, 2020) akiwa tayari amefariki dunia.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya imekiagiza Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Mwanza (Nyanza) kubuni njia muafaka za kujitegemea kiundeshaji kwa kutumia rasilimali nyingi ilizonazo.
Ripoti mpya zilizotolewa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) inaeleza kuwa kuendelea kupungua kwa saa za kazi kutokana na athari za virusi vya Corona (COVID-19) kunazidi kuhatarisha ajira katika sekta isiyo rasmi ambayo ni karibu nusu ya wafanyakazi wote duni
Wagonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) wamefikia 480 nchini Tanzania baada ya Serikali kutangaza ongezeko la wagonjwa wapya 196 leo, kiwango ambacho ni juu zaidi Afrika Mashariki.
Wananchi wa Ubelgiji wameombwa kula chipsi angalau mara mbili kwa wiki kutokana kuwepo zaidi ya tani 750,000 za viazi mviringo ambavyo visipotumika vitatupwa.
hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu, wizara yake imepokea takriban theluthi tatu ya fedha zilizoidhinishwa na Bunge la Tanzania katka bajeti ya mwaka 2019/2020 kiwango ambacho ni cha juu kwa utekelezaji ikilinganishwa na mwaka jana.
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohammed ametangaza ongezeko la wagonjwa wapya saba wa Corona na kufikisha idadi ya wagonjwa 105 visiwani humo.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Ghebreyesus amesema wanaguswa na kuongezeka kwa visa katika baadhi ya mabara ulimwenguni
Ni fedha zilizotolewa na taasisi tatu za Global Fund, Airtel Tanzania na Rotary Club Tanzania.
Sehemu kubwa ya msada huo utatumika kununua vifaa kinga kwa ajili ya watumishi wa afya.
Bei ya jumla ya mahindi katika Mkoa wa Dodoma imeshuka kwa takriban asilimia 44 ndani ya kipindi cha wiki moja, jambo linawapa ahueni wanunuzi wa zao hilo katika mkoa huo uliopo katikati mwa Tanzania.
Waziri huyo ameweka wazi kuwa atachukua hatua kwa taasisi hizo ambazo hakuzitaja kwa majina pale zitakapoendelea kuuza kwa bei zinazojipangia.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amewasamehe na kuwachilia huru wafungwa 833 ili kupunguza msongamano magerezani wakati baadhi ya nchi za Ulaya zikilegeza masharti yaliyowekwa kuzuia kusambaa maambukizi ya ugonjwa wa Corona (COVID-19).
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ameliomba Bunge liidhinishe Sh1.34 trilioni kwa ajili matumizi ya mwaka 2020/2021 ikiwa ni pungufu kidogo kwa asilimia 2.8 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka huu unaoishia mwezi Juni.