Ndugai ahitimisha safari ya miaka tisa ya ubunge wa Lissu
Asema ubunge wa mbunge huyo machachari umekoma baada ya kuvunja masharti ya katiba ya kutooneka bungeni bila taarifa na kutojaza fomu ya maadili ya mali na madeni.
Asema ubunge wa mbunge huyo machachari umekoma baada ya kuvunja masharti ya katiba ya kutooneka bungeni bila taarifa na kutojaza fomu ya maadili ya mali na madeni.
Unawaunganisha wakulima ili kutatua changamoto za kilimo bila kuhitaji maafisa ugani.
Uwekezaji huo umefanyika kupitia taasisi yake ya Vodacom Tanzania Foundation kati ya mwaka 2014 na 2017 katika sekta za kilimo, afya na elimu.
Bajeti hiyo ya Serikali kwa mwaka 2019/20 ya Sh33.1 trilioni imepitishwa baada ya zaidi ya robo tatu ya wabunge waliokuwepo bungeni leo kupigia kura ya “Ndiyo”.
Serikali yajipanga kutokomeza maambukizi mapya kwa kuangamiza mazalia na kuwajengea uwezo wahudumu wa afya.
Amewashauri kuishi kulingana na uwezo wao na kuepuka kukimbilia wasivyoviweza huku ushauri wake ukipokelewa kwa hisia tofauti na vijana.
Mfumo huo utasaidia kuharakisha na kupunguza gharama za utoaji huduma za ardhi ikiwemo utoaji wa hatimiliki za ardhi.
Wabunge wa mkoa wa Njombe wambana Waziri kuhusu kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo wa uchimbaji wa chuma na makaa ya mawe.
Watu waliongezeka ni milioni 1.64 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja na kuifanya Tanzania iwe na watu milioni 54.14.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa amesema Serikali itawahudumia na kuwapeleka katika maeneo yao majeruhi wote wa ajali hiyo.
Fedha hizo zimeokolewa mwaka 2018/2019 baada ya kuanzishwa kwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na zilipaswa zilipwe kwa mawakili binafsi wanaosimamia mashauri ya Serikali.
Amewataka wasiisubiri Serikali kuboresha na kutatua changamoto za wanawake bali watumie kanuni za Bunge kuifanyia marekebisho Sheria ya Mirathi sura 352.
Amewashauri kujiwekea akiba kwa kununua hisa katika taasisi za fedha.
Inakusudia kufanya maboresho ya mfumo na sera ili kufuta na kupunguza baadhi ya kodi, ushuru na tozo.
Waziri wa fedha na mipango amesema msamaha huo umeshindwa kuwanufaisha walengwa na badala yake wafanyabiashara walitumia fursa ya kujiongezea faida.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema hizo ni juhudi za Serikali za kuwasogezea wananchi huduma ya umeme vijijini.
Amesema wastani wa pato la kila mtu uliongezeka kwa zaidi ya Sh130,000 mwaka 2018.
Ripoti mpya iliyotolewa na NBS inasema asilimia 55 ya Watanzania hawana nyaraka zinazothibitisha kuwa wanamiliki ardhi au makazi.
Ni Mwenyekiti, wajumbe wawili wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo na Ofisa Mkuu wa Ufundi (CTO).
Amesema wawakilishi wa kampuni hiyo walikuwa hawayumbishwi na walisimamia walichokiamini, licha ya kuwa maridhiano yamefikia hatua nzuri.