Nane mbaroni kwa wizi wa vifaa vya ujenzi daraja la Magufuli
Jeshi la polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu nane kwa kosa la kuiba vifaa vya ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi (John Magufuli) zikiwemo nyaya.
Jeshi la polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu nane kwa kosa la kuiba vifaa vya ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi (John Magufuli) zikiwemo nyaya.
Rais Samia Suluhu Hassan amesema yeye na watu waliohudhuria mkutano wa wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam wameamua kuvaa barakoa ili kuwakinga wazee dhidi ya ugonjwa wa Corona ambao unaitesa dunia kwa sasa.
Tahadhari ya kunawa mikono kwa maji na sabuni na kutumia vitakasa mikono ili kujikinga na ugonjwa wa Corona imeleta matokeo chanya baada ya kusaidia kupunguza magonjwa ya mlipuko kikiwemo kipindupindu katika Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.
Rais Samia Suluhu Hassan amesema uhusiano wa Tanzania na Kenya haupaswi kujengwa katika misingi ya ushindani na uhasama badala yake ujikite katika undugu.
Rais Samia Suluhu Hassan amesema ziara yake nchini Kenya iliyoifanya kwa siku mbili ndiyo ziara yake kwanza tangu alipoteuliwa kuwa Rais wa sita wa Tanzania Machi 19 mwaka huu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anahutubia Bunge la Kenya lililo na mjumuiko wa wabunge wa Seneti na Bunge la Kenya.
Rais Samia Suluhu Hassan amesema amefanya mazungumzo na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ambapo wamekubaliana mambo mbalimbali ikiwemo kukuza na kuimarisha uhusiano na mshikamano kati ya mataifa hayo mawili.
Wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu Tanzania wameanza mwezi Mei kwa neema zaidi kutokana na kuendelea kupunguziwa maumivu baada ya Serikali kutangaza kuondoa asilimia 10 ya faini kwa wale wanaochelewa kuanza kurejesha fedha hizo.
Anatarajiwa kuhutubia kikao cha pamoja cha Bunge la Kitaifa na Seneti kesho.
Ameingia kwenye orodha vigogo wanaongoza taasisi za fedha na bima baada ya kuteuliwa kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya huduma za bima ya Jubilee Insurance.
Wadau wa habari wasema uhuru wa habari Tanzania umeporomoka hasa kipindi cha miaka ya hivi karibuni.
Imeipongeza kwa mchango wake wa kukabiliana na habari za uzushi kwa kutoa mafunzo ya uthibitishaji habari na ujuzi wa kidijitali kwa waandishi wa habari na vijana wa Tanzania.
hadi kufikia Machi mwaka huu imefanikiwa kuzalisha na kusambaza vitambulisho vya Taifa milioni 7.1, licha ya kugawa namba za utambulisho (NIN) milioni 18.7 kwa wananchi, jambo linalowaacha mamilioni ya Watanzania bila vitambulisho.
Serikali imesema itawachukulia hatua watumishi watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo ya umma.
Rais Samia Suluhu Hassan leo ametangaza kuwa Serikali imepunguza kodi ya mshahara hadi kufikia asilimia nane huku akiahidi kupandisha mishahara ya wafanyakazi mwakani.
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuwataka baadhi ya vijana wa kujitolea waliochaguliwa kujiunga na jeshi hilo mwaka 2020/21 kuripoti tena jeshini baada ya kurejeshwa nyumbani mwezi Februari mwaka huu.
Itafanya mapitio ya mitaala ya shule za msingi na sekondari ili kuingiza stadi mbalimbali za maisha zitakazowasaidia wahitimu kuwa na uwezo wa kiushindani katika soko la ajira.
Vifaa hivyo vinavyotumiwa na mtu binafsi kujipima Virusi Vya Ukimwi (VVU) sasa vitauzwa chini Sh4,600 duniani.
Serikali imewataka waajiri kote nchini kuweka mifumo madhubuti ya usalama mahala pa kazi ili kuwakinga wafanyakazi na kuwalinda na hatari zinazoweza kutokea wanapotekeleza majukumu yao ya kazi.
Makamu wa Rais Dk Philip Mpango amesema Serikali iliamua kutokufanya sherehe za Muungano wa Tanzania mwaka huu kutokana na tukio la hivi karibuni la kifo cha Hayati Rais John Magufuli.