Live: Safari ya mwisho ya Hayati John Magufuli
Viongozi na waombolezaji mbalimbali leo wanashiriki shughuli ya maziko ya Hayati Rais John Magufuli.
Viongozi na waombolezaji mbalimbali leo wanashiriki shughuli ya maziko ya Hayati Rais John Magufuli.
Mchakamchaka wa wananchi walioamua kusindikiza mwili wa Hayati Rais Magufuli ni mkubwa kiasi cha kutokuweza kuona mwisho wake.
Mkuu wa mkoa asema wanaweza kukaa nyumbani na kufuatilia kwenye runinga ili kuwaepusha na madhira ya msongamano
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema anamfahamu binafsi hayati Rais John Magufuli kama kiongozi mchapakazi, mfuatiliaji, mnyenyekevu, mwalimu na aliyekuwa na maono makubwa ya kuboresha maisha ya Watanzania.
Rais wa sita wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kwa wale ambao wana mashaka kuwa anaweza kuwa rais, wafahamu kuwa yeye ni Rais mwenye maumbile ya mwanamke.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema sasa mwili wa Hayati Rais Magufuli utazungushwa uwanjani na mitaani badala ya kila mwananchi kupita mbele ya jeneza.
Mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli unaagwa leo na viongozi, wabunge na wananchi wa Jiji la Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amewataka wakazi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kumuaga Hayati Rais Magufuli katika uwanja wa CCM Kirumba Machi 24 mwaka huu.
Mwili utaanza kuagwa Dar es Salaam kwa siku mbili, Dodoma, Zanzibar, Mwanza na kisha Geita.
Wakazi wa maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar es Salaam wamejitokeza katika barabara ambapo mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli ulipopita kuelekea katika uwanja wa Uhuru.
Leo Machi 20, 2021 mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Magufuli unaagwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Ni ujenzi wa miundombinu ya barabara, madaraja, kiwanja cha ndege na meli ambayo imerahisisha shughuli za biashara na usafirishaji kwa wakazi wa jiji hilo.
Amewataka Watanzania kujenga umoja, kuzika, tofauti zao na kuwa na matumaini wakati Serikali ikitafuta namna ya kuwekana sawa kuhusu mambo muhimu ya Taifa.
Mwili wa Hayati Dk John Magufuli unatarajiwa kupumzishwa katika nyumba yake ya milele wilayani Chato katika Mkoa wa Geita Machi 25 mwaka huu.
Samia Suluhu Hassan ameapa rasmi na kuwa Rais wa sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa ndiyo mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo wa juu katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Msemaji Mkuu wa Serikali Dk Hassan Abbasi amesema Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kulihutubia Taifa Ijumaa ya Machi 19 kuhusu taratibu na ratiba nzima ya mazishi ya hayati Dk John Magufuli.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amewataka wakazi wa mkoa huo kujitokeza katika ibada maalum ya kumuombea Hayati Rais John Magufuli itakayofanyika katika uwanja wa Sokoine kesho Machi 19, 2021.
Viongozi mbalimbali duniani na jumuiya za kimataifa zimetoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Rais John Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Iliongea hadharani Februari 26, 2021 wakati wa uzinduzi wa majengo ya Chuo Cha Polisi kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam.
Alikuwa amelazwa katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.