Wanafunzi wasioona wanavyosaka elimu ya sayansi kama dhahabu Tanzania
Hali yao inawalazimu kusoma masomo ya sanaa hivyo ndoto zao kuishia angani.
Hali yao inawalazimu kusoma masomo ya sanaa hivyo ndoto zao kuishia angani.
Ugonjwa huo uliolipuka nchini China mwishoni mwa Desemba 2019 unaendelea kuwatesa wafanyabiashara ambao wanategemea nchi hiyo kwaajili ya manunuzi ya bidhaa zao.
Uzalishaji wa mazao ya ufuta umeshuka kwa zaidi ya mara nne hadi kufikia tani milioni 1.6 mwaka 2018 ukichagizwa na ukosefu wa soko la uhakika na bei ya kuridhisha kwa mazao hayo ambayo yamekuwa yakitumika katika uzalishaji mafuta ya kula nchini.
Matunda ya stroberi yana matumizi mbalimbali kulingana na uhitaji wa mtumiaji, jamii na maeneo ikiwemo kuliwa kama tunda, ladha katika aina mbalimbali za vyakula, kuweka rangi, harufu na nakshi katika vipodozi na kutengeneza marashi.
Vijana waliowekeza na wanaotaka kuwekeza katika ufugaji wa samaki Tanzania wametakiwa kuchukua tahadhari na kutumia vizuri ujio wa mvua za masika kuongeza uzalishaji utakaowasaidia kuongeza fursa za ajira na kipato cha kuendesha maisha yao.
Baadhi ya waajiri hutumia fursa hiyo kutimiza matakwa yao na kuwaacha waliojiunga na programu hizo wakihangaika bila kutimiza malengo yao.
Licha ya umuhimu wa vyama vya kutetea maslahi ya wafanyakazi, bado mwitikio wa wafanyakazi vijana kujiunga katika vyama hivyo ni mdogo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa hamasa na elimu.
Wakati wengine wakiona funza kama uchafu, Katala ambaye ni Mtanzania anayesoma katika Chuo cha Afrika cha Uongozi (ALU) kilichopo nchini Rwanda, kwake hiyo ni fursa ya kuboresha maisha yake na jamii.
Baada ya kukuletea makala mbalimbali za mambo yanayohusu ajira Tanzania, leo tena tunaendelea kuliangalia suala hilo kwa mapana hasa fursa wanazoweza kuzitumia vijana ambao bado hawajapata kazi.
Ni muda mzuri wa kuangalia fursa zingine zitakazosaidia kuboresha maisha nje ya kazi unayofanya.
Wameshauriwa kuwa wavumilivu na watatuzi wa changamoto na mazingira yasiyoridhisha ya kazi ili kuaminiwa na waajiri wao.
Zipo sababu mbalimbali ambazo zinawasukuma waajiri wengi kutokutoa mrejesho kwa kila mwombaji wa kazi ambaye hajafanikiwa kuitwa kazini ikiwemo kuwapunguzia waombaji msongo wa mawazo.
Baadhi yao hukosa kujiamini, kujieleza, mvuto na utashi wa vitu walivyoviandika kwenye wasifu (CV), jambo linalowakosesha kazi kila wanapoitwa kwenye mahojiano.
Baadhi ya makosa hayo ni matumizi yasiyo sahihi ya barua pepe na kukosa umakini wakati kutuma maombi ya kazi.
Tenga muda wa kujifunza na kupata taarifa ya kinachoendelea katika sekta ya ajira. Tambua soko linahitaji nini kwa wakati huu ukilinganisha na ulichonacho.
Programu za ujuzi, ufundi stadi zinawaweza kupunguza tatizo la ajira nchini.
Alipata msamaria mwema aliyemwanzishia biashara ya kuuza ice cream baada ya kumkuta akiombaomba Kariakoo
Licha ya kuwa magari yanayotumia gesi asilia yanaokoa uharibifu wa mazingira na gharama za maisga kwa kupunguza gharama za mafuta mafuta, bado muitikio wa Watanzania kutumia magari hayo ni mdogo.
Wamiliki wa vyombo vya moto wanaweza kupunguza gharama za uendeshaji wa vyombo hivyo kwa takriban asilimia 50 ikiwa watageukia matumizi ya gesi asilia kuendesha magari yao na kuchangia katika utunzaji wa mazingira.
Waliofunga mifumo ya gesi asilia kwenye magari yao wamefanikiwa kupunguza gharama za mafuta wanazotumia kila siku na kuwaletea ahueni ya maisha.