October 6, 2024

Chanjo zilizo mstari wa mbele kupambana na Corona duniani

Chanjo hizi zimetengenezwa katika nchi mbalimbali ikiwemo Marekani na Ujerumani.

  • Zimetengenezwa nchi mbalmbali ikiwemo Marekani na Ujerumani.
  • Chanjo hizo zimetofautiana kiwango cha ufanisi wake katika kupambana na Covid-19.

Dar es Salaam. Utolewaji wa chanjo ya ugonjwa wa Corona ni kati ya sehemu ambazo zimekuwa na habari za uzushi katika mitandao ya kijamii.

Video, picha na sauti zimekuwa zikizunguka katika mitandao ya kijamii zikiongelea mazuri, mabaya na yasiyojulikana kuhusu chanjo ya ugonjwa wa Corona.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) limeainisha chanjo maarufu ambazo zimeidhinishwa kupambana na Corona na ambazo zimeanza kuleta matokeo mazuri licha ya kuwa maambukizi ya ugonjwa huo yanaongezeka kila siku.

Tazama video hii kuzifahamu chanjo hizo ikiwemo ya Oxford/AstraZeneca ambayo ndiyo inasambazwa katika maeneo mengi kupitia programu ya Umoja wa Mataifa ya COVAX.