July 8, 2024

Dhana potofu za kuepukwa baada ya kupata chanjo ya Corona

Hakuna chanjo ya Corona ambayo imetolewa na kuthibitishwa kufanya kazi kwa asilimia 100 kwa watu waliopata chanjo hiyo hivyo tahadhari hata baada ya chanjo ni muhimu.

  • Ni kufikiri kuwa kupata chanjo ndiyo mwisho wa kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.
  • Baada ya chanjo endelea kuchukua tahadhari ikiwemo kunawa mikono na kuvaa barakoa.

Dar es Salaam. Baadhi ya watu wanafikiri wakipata chanjo ya Corona hawatakiwi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.

Wanafikiri ndiyo mwisho wa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, kuvaa barakoa na ndiyo mwanzo wa kuanza kukusanyika kama ilivyokuwa miaka mitano iliyopita.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), hakuna chanjo ya Corona ambayo imetolewa na kuthibitishwa kufanya kazi kwa asilimia 100 kwa watu waliopata chanjo hiyo.

Ni sawa na kusema haujahakikishiwa kuwa usipochukua tahadhari dhidi ya Corona kisa umepata chanjo, hautaupata ugonjwa huo bali utakuwa katika upande salama zaidi kuliko ambaye hajapata chanjo kabisa. 

Licha ya kupata chanjo dhidi ya Corona, WHO inashauri kuendelea kuchukua tahadhari kwa kufuata kanuni za afya zilizotolewa dhidi ya ugonjwa huo unaoendelea kusumbua watu duniani.

Jifunze zaidi kwa kutazama video hii: