October 6, 2024

Dhana potofu zinawazuia baadhi ya watu kujikinga na Corona

Ni pamoja na kuamini kuwa watoto hawawezi kupata Corona na kuwa kuvaa barakoa kunasababisha ukosefuwa hewa.

  • Ni pamoja na kuamini kuwa watoto hawawezi kupata Corona na kuwa kuvaa barakoa kunasababisha ukosefuwa hewa.

Dar es Salaam. Ugonjwa wa Corona ni kati ya masuala mtambuka kwa mataifa mengi duniani huku ukiacha majeraha ya moyo baada ya wapendwa wa baadhi ya watu kupoteza maisha.

Hata hivyo, vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Corona bado siyo fundisho kwa baadhi ya watu kwani wengine wameendelea kupuuzia kanuni za kujikinga na ugonjwa huo na hivyo kusababisha kuongezeka kwa maambukizi na idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa huo. 

Hivi karibuni, Mkurugenzi wa huduma za dharura wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dk Michael Ryan alisema, licha ya mataifa mengi kuweka juhudi za kukabiliana na Corona ikiwemo kufunga mipaka na kutoa chanjo, Corona inaweza isitokomezwe lkabisa mwaka huu.

Dk Ryan ameyasema hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari Jijini Geneva nchini Uswisi huku akikiri kushangazwa na kuongezeka kwa idadi ya maambukizi katika nchi mbalimbali zikiwemo Marekani, nchi za Ulaya na Asia.

“Tunafanya kazi zaidi kuelewa hali ya kuongezeka kwa maambukizi. Mengine ni kwa sababu ya kulega kwa kuzingatiwa kwa kanuni za afya ya jamii na watu kuacha kuchukua tahadhari,” amesema Dk Ryan.

Je, ni dhana zipi ambazo huenda zikawa sababu ya kuendelea kuongezeka kwa maambukizi ya Corona? Tazama video hii kujifunza zaidi.