October 7, 2024

Dondoo muhimu kukitunza choo nyumbani

Zitakusaidia kuepukana na madhara ya kiafya na kiuchumi yanayyoambatana na kutokukisafisha choo cha nyumbani kwako.

  • Ni pamojana kuhakkikisha uwepo wa maji muda wote.
  • Usafi wa chooni ufanyike walau mara mbili kwa siku.

Dar es Salaam. Msemo wa nyumba ni choo una maana pana kuliko inavyodhaniwa na baadhi ya watu. 

Choo kikiwa kichafu na kisichokidhi viwango vya ubora na usafi kinaweza kusababisha madhara mengi ya kiafya na kiuchumi kwa wanafamilia. Changamoto zingine ni harufu mbaya na wadudu kama nzi nyumbani.

Unawezaje kukitunza choo chako kuepukana na changamoto hizo? Tazama video hii kujifunza.