November 24, 2024

Dondoo zitazokusaidia wakati wa kupata chanjo ya Corona

Unashauriwa kukaa karibu na kituo cha chanjo walau kwa dakika 15 baada ya kupata chanjo.

  • Ni pamoja na kufahamu kiasi cha dozi unachotakiwa kupewa.
  • Pia unashauriwa kukaa karibu na kituo cha chanjo walau kwa dakika 15 baada ya kupata chanjo.

Dar es Salaam. Wakati nchi mbalimbali zikiendelea kupokea chanjo kwa ajili ya ugonjwa wa Covid-19, changamoto ya kuwepo kwa habari za uzushi kuhusiana na usalama wa chanjo  za Corona nayo imeendelea kuwepo.

Baadhi ya wapotoshaji wanatumia mitandao ya kijamii kama WhatsApp na Instagram kuweka habari zinazopotosha juu ya ugonjwa wa Corona ikiwemo chanjo kuwa ina madhara kwa mpokeaji wake.

Hata hivyo, kwa baadhi ya video, sauti na picha zinazotumika kupotosha, zingine ni za maudhui ambayo yanaonyesha watu wakipitia baadhi ya changamoto tarajiwa baada ya kupata chanjo ikiwemo kutapika na maumivu ya kichwa.

Shirika la Afya Duniani (WHO) kupitia tovuti yake limesema mtu anapopata chanjo anaweza kupatwa na changamoto za muda mfupi ambazo zinasababishwa na mwili kuipokea chanjo hiyo ikiwemo uchovu wa mwili na hata maumivu sehemu ya viungio na misuli.

Kuelewa zaidi, tazama video hii fupi.