July 8, 2024

Faida utakazopata ukiimarisha usafi kwenye mgahawa

Usafi wa mgahawa ni pamoja na kuhakikisha chakula kinachopikwa kinalinda afya za wateja wako.

  • Usafi wa mgahawa ni pamoja na kuhakikisha chakula kinachopikwa kinalinda afya za wateja wako.
  • Kutoa huduma nzuri zenye kuzingatia kanuni zote za afya. 

Dar es Salaam. Huenda wafanya biashara wenye migahawa wanajiuliza maswali mengi juu ya upatikanaji wa wateja katika migahawa yao bila kufahamu sababu ndogo ndogo ambazo humfanya mteja ashindwe kurudi pale anapomaliza kupata huduma ya chakula.

Wadau wa migahawa iliyojizolea umaarufu jijini Dar es Salaam wamesema kuwa wateja hawavutiwi na ladha ya chakula pekee kwani wapo ambao huzingatia afya zao na huanza kwa kuangalia usafi wa mgahawa.

Meneja wa mgahawa wa Akemi uliopo Posta Jijini Dar es Salaam Bishanga Kalaule ameiambia Nukta Habari (www.nukta.co.tz) kuwa usafi wa mgahawa una uhusiano wa moja kwa moja na wateja wanaokuja kupata huduma.

“Leo ukipata wateja 100, lengo kuu ni kuhakikisha kuwa 100 wote wanarudi kesho. Endapo mgahawa wako upo katika hali ya kuvutia lazima wataambizana na utapata wateja wengi,” amesema Kalaule.

Ni muhimu kwa wamiliki wa migahawa kufahamu kuwa usafi wa mgahawa siyo tu katika eneo la kuuzia chakula lakini huanzia sokoni wakati wa manunuzi. Je, kuna faida gani zingine za usafi katika mgahawa? Tazama video hii kufahamu zaidi.