November 24, 2024

Fidia ya wahanga wa ajali ya ndege ya Boeing 737 Max 8 yaibua nongwa

Kampuni inayotengeneza ndege ya Boeing imeanza mchakato wa kuzilipa fidia familia za watu waliopoteza maisha katika ajali mbili za ndege aina ya Boeing 737 Max 8 zilizotokea Indonesia na Ethiopia mwaka huu lakini familia hizo zimesema kiasi kilichopangwa k

  • Ndege hizo zilikuwa zinamilikiwa na masharika ya ndege ya Ethiopia Airlines  na Indonesia (Lion Air) zilianguka kwa nyakati tofauti na kuua watu 346. 
  • Kampuni ya Boeing imetenga Sh332.04 milioni kwa kila familia iliyopoteza ndugu. 
  • Baadhi ya familia zinahoji ulinganifu wa pesa hiyo na pengo lililoachwa na wapendwa wao waliofariki.

Dar es Salaam. Kampuni inayotengeneza ndege ya Boeing imeanza mchakato wa kuzilipa fidia familia za watu waliopoteza maisha katika ajali mbili za ndege aina ya Boeing 737 Max 8 zilizotokea Indonesia na Ethiopia mwaka huu. 

Ndege hizo zilikuwa zinamilikiwa na masharika ya ndege ya Ethiopia Airlines  na Indonesia (Lion Air) zilianguka kwa nyakati tofauti kutokana na hitilafu za kiufundi na kuua watu 346. 

Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo,  inatarajia kuilipa kila familia takribani Sh332 milioni ambazo zimetokana na mfuko wa msaada wenye kiasi cha Sh 114.9 bilioni uliotangazwa hivi karibuni. 

Boeing yenye makao makuu nchini Marekani imeanza kupokea malalamiko ya familia za waliofariki katika ndege hizo na yanatakiwa yawasilishwe kabla ya 2020 ili yaanze kufanyiwa kazi. 

Hata hivyo, baadhi ya familia, kwa mujibu wa duru za kimataifa zimesema kiasi hicho kinachotolewa na Boeing ni kidogo na hakiwezi kuziba pengo la lililoachwa na wapendwa wao. 

Ndege za 737 Max zimezuiwa kuruka tangu Machi mwaka huu wakati uchunguzi ukiendelea kufanyika dhidi ya usalama wa ndege hizo kufuatia ajali zilizotokea Indonesia na Ethiopia. 

Awali, Boeing iliahidi kutoa  Sh299 bilioni kwa familia na jamii zilizoathirika na ajali hizo.

Ndege hizo zilikuwa zinamilikiwa na masharika ya ndege ya Ethiopia Airlines  na Indonesia (Lion Air) zilianguka kwa nyakati tofauti kutokana na hitilafu za kiufundi na kuua watu 346. Picha|Mtandao.

Taarifa ya kampuni hiyo iliweka wazi kuwa nusu ya pesa hizo zingetumika kufanya malipo ya moja kwa moja kwa familia huku nusu yake ikielekezwa kwenye elimu na shughuli za maendeleo kwenye jamii zilizoathirika na ajali za ndege zake.

Robert Clifford ambaye aliongoza shauri la Shirika la ndege la Ethiopia amesema kukosekana kwa taarifa za kina kipindi matangazo hayo yanafanyika ni mipango ya Boeing kupoza wananchi na kuepusha maswali ya kiusalama dhidi yake.


Zinazohusiana


Hata hivyo, katika taarifa yake, Mkurugenzi Mkuu wa Boeing,  Dennis Muilenberg aMEsema ufunguzi wa mfuko huo ni hatua kubwa kwenye jitihada za kampuni hiyo kusaidia ndugu wa marehemu waliofariki, licha ya kuwa kuna hiari ya kushiriki kwenye mfuko huo.

Familia zitakazowasilisha maombi ya kupatiwa fidia hazitapata tena haki ya kufungua kesi nyingine ya madai baada ya kupata fedha hizo.