Hawa ndiyo marapa 10 wenye mkwanja mrefu duniani
Orodha hiyo imeongozwa na msanii Kanye West ambaye anamiliki Sh344.7 bilioni akitawaliwa na wanaume ambo wote wanatoaka nchini Marekani.
- Orodha hiyo imeongozwa na msanii Kanye West ambaye anamiliki Sh344.7 bilioni.
- Tano bora ya wasanii hao inashikiliwa na Jay Z, Diddy, Drake,Travis Scott na West.
- Marapa wote wanatoka nchini Marekani.
- Hakuna msanii wa kike aliyeingia 10 bora lakini Nicki Minaj na Cardi B wamefanikiwa kuingia kwenye 20 bora.
Dar es Salaam. Siku chache zilizopita, jarida la Forbes limewataja wanamuziki wa HipHop ambao wanalipwa mkwanja mrefu zaidi duniani huku orodha hiyo ikionyesha mabadiliko baada ya mapinduzi makubwa kufanyika ikilinganishwa na mwaka 2018 na hata 2017.
Sura mpya zimeingia kwenye 10 bora huku baadhi ya wakongwe waliokuwepo katika orodha hiyo kuondolewa baada ya mapato yao kupungua.
Hii ndiyo orodha ya wanamuziki 10 wa HipHop wenye utajiri mkubwa kwa mwaka 2019 iliyotolewa na jarida hilo ambao wote wanatoka Marekani:
10. Donald Glover (Childish Gambino)
Gambino ambaye hakuiona orodha hii mwaka jana amefanikiwa kuingia baada ya kumiliki kiasi cha Sh80.4 bilioni. Gambino aliyewika na wimbo wa “This is America” na kuigiza filamu ya Guava Island na Lion king ni kati ya wasanii wenye namna yao ya pekee kwenye muziki.
Gambino (35) ambaye ni raia wa Marekani ni muigizaji, mchekeshaji, mtayarishaji wa muziki, Dj na mwanamuziki wa miondoko ya hiphop na wakati mwingine RnB.
Kundi hili lenye marapa watatu kutoka Marekani (Offset, Takeoff na Quavo) lililoanzishwa mwaka 2008 na kutamba zaidi na wimbo wa “Bad and Boujee”. limeingia katika orodha hiyo ya dhahabu baada ya kumiliki Sh82.7 bilioni kwa mwaka 2019.
Wamepanda nafasi tatu ukilinganishwa nafasi ya 13 waliyoshikilia mwaka jana kwa kuwa na kitita cha Sh56.3 bilioni.
Lamar (32) ni rapa wa Marekani ambaye pia ni mtengenezaji na mwandishi wa nyimbo. Amewahi kutajwa na gazeti la Time la Marekani kama mmoja kati ya watu 100 wenye ushawishi zaidi duniani.
Kwenye orodha hii, Lamar ameporomoka nafasi 5 baada ya kutoka nafasi ya 3 mwaka jana ambapo alimiliki Sh133.3 bilioni hadi nafasi ya nane mwaka huu ambapo anamiliki Sh88.5 bilioni.
Lamar ametamba zaidi na kibao chake cha “Humble” na “All the Stars” ambayo ilikuwa ni nyimbo rasmi (Theme Song) kwenye filamu ya Black Panther.
Lamar ameporomoka nafasi 5 baada ya kutoka nafasi ya 3 mwaka jana ambapo alimiliki Sh133.3 bilioni hadi nafasi ya nane mwaka huu ambapo anamiliki Sh88.5 bilioni. Picha| Mtandao.
7. DJ Khaled
Ongezeko la Sh29.8 bilioni limemtoa Khaled nafasi ya 11 kwa mwaka 2018 hadi nafasi ya saba mwaka huu baada ya kumiliki Sh91.9 bilioni.
Khaled Mohamed Khaled, anayejulikana zaidi kama DJ Khaled, ni DJ wa Marekani, mwandishi na mtengenezaji wa nyimbo, mtayarishaji na mtangazaji wa vipindi vya redio.
Mzaliwa huyo wa New Orleans, Louisiana, alipata umaarufu kama mtangazaji wa radio miaka ya 1990 kwenye kituo cha Hiphop cha Miami 99 Jamz.
6. Eminem
Baada ya kurekodiwa kuwa na Sh52.8 bil na kushika nafasi ya 13 mwaka 2018, Marshall Bruce Mathers III ama anayejulikana kama Eminem (46) amefikia mkwanja wa Sh114.9 bilioni mwaka huu na kumfanya rapa huyo kushika nafasi ya sita.
Rapa huyo naye anatoka Marekani ametamba zaidi na wimbo wa “Love the way you lie” aliomshirikisha Rihanna na wimbo mwingine wa “Not afraid”
Zinazohusiana
5. Travis Scott
Jacques Berman Webster au akijulikana kama Travis Scott ana mkwanja wa Sh133.2 bilioni ambao umemuweka kwenye nafasi tano kwa mwaka 2019 baada ya kushikilia nafasi ya 15 kwa mwaka 2018 alipokuwa na utajiri wa Sh48.2 bilioni.
Kabla ya nafasi hiyo kushikiliwa na rapa huyo wa Marekani, mwaka 2018, nafasi hiyo ilikaliwa na J Cole ambaye ameporomoka hadi nafasi ya 11.
Scott ni mwandishi na muandaaji wa muziki, mbali na Hiphop anaimba nyimbo za aina nyingine.
4. Diddy
Msanii huyu amewahi kalia kiti cha enzi mwaka 2017 alipomiliki Sh298.7 bilioni na kushika nafasi ya pili kwa kumiliki Sh1.9 trilioni mwaka jana kabla ya kushuka hadi nafasi ya nne mwaka huu ambapo anamiliki Sh160.8 bilioni.
Diddy (49) ambaye jina lake halisi ni Sean John Combs pia ni mwimbaji, mmiliki wa lebo ya muziki ya Bad Boy Entertainment, mwandishi na mtengenezaji muziki.
3. Drake
Aubrey Drake Graham (32) almaarufu kama Drake ni rapa wakimarekani alietamba na wimbo wa “Hotline bling” wenye watizamaji zaidi ya bilioni kwenye mtandao wa YouTube.
Akiwa amepanda kutoka nafasi ya 4 kwa mwaka jana, Drake ametoka kwenye kumiliki Sh107.9 bilioni hadi Sh172.3 milioni kwa mwaka huu. Kati ya mafanikio makubwa ya msanii huyu ni pamoja na kuwa msanii aliyetafutwa na kufuatiliwa zaidi kwa mwaka 2018 baada ya watu 8.2 bilioni kumfuatilia.
Drake ni mfanya biashara, mwanamuziki, mwandishi wa nyimbo na mwigizaji lakini pia anapenda kufuatilia mchezo mpira wa kikapu.
Aubrey Drake Graham (32) almaarufu kama Drake ni rapa wakimarekani alietamba na wimbo wa “Hotline bling” wenye watizamaji zaidi ya bilioni kwenye mtandao wa YouTube. Picha|Mtandao.
2. Jay Z
Baada ya Shawn Carter maarufu kama Jay Z kushika nafasi ya kwanza mwaka 2018 kwa kumiliki Sh2.06 trilioni, mwaka huu ameshika nafasi ya pili kwa kumiliki kiasi cha Sh186.1 bilioni kwa mwaka huu.
Jay Z (49) ametamba zaidi na wimbo wake wa “Story of O.J” ambao umempa umaarufu mkubwa duniani.
Jay Z ambaye pia ni mume wa Beyonce hajafanya mizunguko mingi mwaka huu na kwa mujibu wa wadau wa muziki huo, hicho ndyo chanzo cha kuporomoka kwake.
1. Kanye West
Akiwa ni mume wa Kim Kardashian, ni mwana Hiphop mdogo zaidi kuwahi kukalia nafasi hii miaka mitatu iliyopita.
Mapinduzi yaliyofanywa na rapa huyu ni makubwa kwani amepanda kutoka nafasi ya 10 ambapo alimiliki Sh63.1 bilioni hadi kufikia nafasi ya kwanza akiwa anamiliki Sh344.7 bilioni.
Forbes imeweka wazi kupanda kwa West hadi nafasi ya kwanza kumechochewa na “brand” yake ya viatu vya Yeezy pamoja na nguo zenye brand hiyo.
West mwenye umri wa miaka 42 cheo cha rapa pekee hakikumtosha; ni mwandishi wa nyimbo, mjasiriamali na mbunifu wa mavazi.
West mwenye umri wa miaka 42 cheo cha rapa pekee hakikumtosha; ni mwandishi wa nyimbo, mjasiriamali na mbunifu wa mavazi. Picha| Mtandao.
Wanawake nao hawakuwa mbali kwenye orodha ya Forbes kwani ni Nicki minaj na Cardi B pekee ndio walioingia kwenye 20 bora ya Forbes. Nicki ambaye ametangaza kustaafu hivi karibuni ameshika nafasi ya 12 kwa kumiliki Sh66.6 bilioni.
Nicki amefukuziwa na mwenzie Cardi B ambaye ameshika nafasi ya 13 baada ya kumiliki mkwanja wa Sh64.3 bilioni.
Hata hivyo, baadhi ya wasanii wakiwemo Cardi B na Meek Mill wamehoji juu ya uthabiti wa orodha hiyo kupitia mtandao wa twitter.
Cardi amenukuliwa akihoji “ni wapi Forbes wanapata hizi namba” na hivyo kuzua mijadala juu ya ukweli wa taarifa zinazotolewa na jarida hilo.
Where do Forbes be getting they numbers from cause they way off ?🧐
— iamcardib (@iamcardib) September 19, 2019