July 8, 2024

Hii ndiyo mito mikubwa zaidi Tanzania

Mito hiyo inatumika kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo uvuvi na kilimo lakini inatumiwa kama mipaka inayotenganisha Tanzania na nchi zingine.

  • Mito Ruvuma, Malagarasi, Kagera, Mara na Umba ndio mito mikubwa Zaidi Tanzania.
  • Inatumika kwa shughuli mbalimbali za uvuvi na kilimo.

Dar es Salaam. Tanzania imebahatika kuwa na rasilimali nyingi za asili ikiwa ni pamoja na milima, maziwa, hifadhi za wanyama, mapori ya akiba, mito na mengine mengi yanaifanya kuwa na utajiri wenye kuvutia. 

Kama ulikuwa hufahamu mito mikubwa iliyopo Tanzania, www.nukta.co.tz ipo kwa ajili ya kukuhabarisha na kukujulisha mito hiyo.

Uchambuzi wa ripoti ya Takwimu za Mazingira ya Taifa (National Environment Statistics Report, 2017) zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) zinaonyesha kuwa mito ya Ruvuma, Malagarasi, Kagera, Mara na Umba ndiyo mito mikubwa zaidi.

Mito hiyo inatumika kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo uvuvi na kilimo lakini inatumiwa kama mipaka inayotenganisha Tanzania na nchi zingine.