July 3, 2024

Huduma za nyongeza zinazoweza kufanikisha biashara yako

Ni huduma za kiubunifu ambazo zinaweza kuwavutia wateja kuendelea kutumia huduma au bidhaa zako.

  • Ni huduma za kiubunifu ambazo zinaweza kuwavutia wateja kwa namna fulani.
  • Inaweza kuwa ofa, bonasi, zawadi na kadhalika.

Dar es Salaam. Hakuna biashara au huduma ambayo unafanya peke yako. Wapo washindani ambao nao wanafanya kila namna kuwavutia wateja katika biashara.

Wakati mwingine anatoa huduma ya maji ya moto ya kunawia katika mgahawa wake, mwingine anatoa huduma ya ofa katika vyakula vyake ili kuvutia wateja zaidi. Ni ubunifu tu.

Cha kuzingatia na kuelewa ni kuwa, zipo huduma za nyongeza katika biashara ambazo huwavutia wateja na hivyo kuwafanya waendelee kuhitaji huduma au bidhaa yako. 

Waliopanda “School bus” husema, “it is the little things” wakimaanisha ni vile vitu unavyoviona ni vidogo ndiyo huwa na maana kubwa kwa watu hata katika biashara.

Je, huduma hizo  ni zipi? Tazama video hii kujifunza zaidi.