October 8, 2024

Huwa unamlipa kiasi gani mfanyakazi wako wa ndani kwa mwezi?

Kima cha chini cha wafanyakazi wa ndani hutolewa kulingana na aina mwajiri aliyemwajiri.

Dar es Salaam. Unafahamu kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi wa ndani Tanzania? 

Takwimu muhimu za Tanzania za mwaka 2018 zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) zinaeleza kuwa wafanyakazi wa ndani wasiokaa kwa mwajiri nje ya wale wanaofanya kazi kwa mabalozi, wafanyabiashara na maofisa wenye hadhi, ndio wanaolipwa kima cha chini zaidi kuliko wafanyakazi wengine wa ndani cha Sh80,000 kwa mwezi.