Ifahamu chanjo ya AstraZeneca
Ni chanjo yenye matoleo mawili dhidi ya virusi vya Corona.
- Ni chanjo yenye matoleo mawili dhidi ya virusi vya Corona.
- Inatengenezwa Korea Kusini na india.
- Inatumika kwa matumizi ya dharura.
Dar es Salaam. Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limeizinisha matoleo mawili ya chanjo aina ya AstraZeneca / Oxford dhidi ya virusi vya Corona ambayo imekuwa ikitumika hasa kwa matumizi ya dharura.
Chanjo hiyo ni miongoni mwa chanjo sita zilizoizinisha na shirika hilo katika jitihada za kupambana na ugonjwa wa Uviko-19 hapa duniani.
Aina ya kwanza ya chanjo hiyo inayojulikana kama AstraZeneca-SKBio imetengenezwa nchini Korea Kusini na ya pili ya AstraZeneca / Oxford imetengenezwa na taasisi ya Serum ya nchini India.
Chanjo hiyo imeidhinishwa na WHO kwa matumizi ya dharura kutokana na ufanisi wake wa kuleta matokeo mazuri katika maeneo yenye uhitaji mkubwa wa chanjo.
Hata hivyo, kama ilivyo kwa chanjo zingine usambazaji wake ni mdogo hivyo kipaumbele kimetolewa kwa wafanyakazi wa afya walio katika hatari kubwa ya kuambukizwa na wazee walio na umri wa miaka 65 au zaidi.
Chanjo hiyo inafaa wa kina nani?
Chanjo hiyo inaweza kutolewa kwa ambao wako hatarini kupata Covid-19 kama wenyewe magonjwa ya kisukari, magonjwa ya moyo na upumuaji. Huku watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi bado hawajatajwa kwa sababu tafiti zinaendelea.
Pia chanjo hiyo inaweza kutolewa kwa watu ambao walikuwa na Covid-19 hapo zamani.
Wakina mama wanaonyonyesha na wajawazito nao wanaweza kupatiwa chanjo hiyo, iwapo chanjo hiyo ikiwa wako katika hatari ya kupata Uviko-19 baada ya kupata ushauri wa daktari.
WHO inaeleza kuwa baada ya mama aliyepatiwa chanjo, hatakiwi kuacha kumnyonyesha mtoto wake.
Chanjo hiyo haijapendekezwa kwa watu walio chini ya umri wa miaka 18 pia wale wenyewe mzio.
Ufanisi wa kuleta matokeo kwa mtu aliyepata chanjo hiyo ni asilimia 63.09.
Licha ya kuidhinishwa na WHO, pia mamlaka mbalimbali duniani ikiwemo Wakala wa Dawa barani Ulaya (EMA), Kamati ya Ushauri ya Usalama wa Chanjo Duniani nazo zimeithibitisha chanjo hiyo kutumiwa na watu.
AstraZeneca / Oxford imesambazwa karibu katika nchi zote barani Afrika ikiwemo za Afrika Mashariki za Kenya, Uganda, na Rwanda.