November 24, 2024

Jinsi Google inavyoweza kukupatia taarifa sahihi za Corona

Wakati huu wa janga la Corona, watu wanahitaji taarifa sahihi zitakazowasaidia kuushinda ugonjwa huo kwa kutumia mifumo ya teknolojia.

  • Unaweza kutafuta taarifa ndani ya tovuti kwa haraka na kwa urahisi ili mradi unafahamu vikoa vya taasisi mbalimbali.
  • Ukiweza kufahama vifupi vya mafaili utweza kupata taarifa nyingi ikiwemo za takwimu kwa muda mfupi.

Dar es Salaam. Kitafutio cha vitu mtandaoni cha Google kimekuwa ni nyenzo muhimu kwa watu kupata taarifa na maarifa mtandaoni.

Hata hivyo, siyo kila mtu anaweza kutumia kwa ufanisi kitafutio hicho ambacho kinamilikiwa na kampuni ya Google ya Marekani kwa sababu kina vipengele vingi.

Wakati huu wa janga la Corona, watu wanahitaji taarifa sahihi zitakazowasaidia kuushinda ugonjwa huo kwa kutumia mifumo ya teknolojia.

Leo tunaangazia kwa undani jinsi unavyoweza kutumia kitafutio cha “Google Search” kwa urahisi na kupata taarifa za Corona ambazo zimefichika. Mbinu hizi zinaweza kukusaidia:

Kutafuta ndani ya tovuti

Kwa kutumia mbinu ya kutafuta taarifa katika tovuti sahihi au inavyofahamika kwa lugha ya Kiingereza “serach within the site”. Hapa mtufutaji ataweza kupata taarifa yoyote katika mtandao husika,

Kwa Tanzania, taasisi za umma zote vikoa vyake huwa ni go.tz huku shule na vyuo vikuu ikiwa ni ac.tz, mashirika na kampuni binafsi ikiwa ni co.tz. Mfano, corona Tanzania: www.afya.co.tz.

Google ikitumika vizuri ni nyenzo muhimu ya kupata taarifa sahihi kuhusu Corona. Picha|Mtandao.

Kutafuta kwa kutumia aina ya mafaili

Aina nyingine ya kutafuta taarifa kwa urahisi kwenye mtandao wa Google ni kwa kupitia aina ya mafaili. Kama unataka kupata taarifa ya corona na kujua idadi ya takwimu za  wagonjwa au vifo  anaweza kupata hivyo kwa haraka zaidi akijua tu vifupi vya hayo mafaili.

Ikumbukwe mara zote takwimu hutuzwa kwenye Excel na kifupi chake ni Xls, huku “miscrosoft word” kifupi chake kikiwa ni doc vifupi vingine ni pdf na ppt.

Kwa hiyo kwa mtafutaji wa taarifa hapo juu atatakiwa kufuata kanuni nyepesi kabisa anapotaka kutafuta taarifa. Anatakiwa kuandika taarifa anayotaka kisha ataweka doti tatu ikifuatiwa na aina ya file. Mfano hali ya corona nchini Kenya:.Xls.


Zinazohusiana:


Kuepuka taarifa usizozitaka

Njia nyingine ya utafutaji ni ya kuondoa kitu ambacho hutaki kionekane pale unapotaka kutafuta taarifa ya kitu fulani  katika mtandao wa Google. Hii inawezekana kwa kutumia alama ya  “ – ”.

Alama hiyo ina maanisha katika utafutaji wako wa taarifa katika mtandao wa Google hutaki habari fulani itokee. Mfano unataka habari za kuhusu chanjo ya corona barani Ulaya ila utaki za Afrika zitokee unachofanya nikuandika neno unalotaka litokee kisha unaweka hiyo alama kwa kuambatanisha na neno ambalo hutaki litokee.

Mfano, habari za chanjo ya corona ulaya  -Afrika.

Pia kwa kutumia neno inurl: hapa mtafutaji ataweza kupata taarifa husika zenye chanzo anachokitaka kutoka katika taasisi husika kupitia kiunganishi au “link”.

Mfano akiandika neno inurl: katika mtandao wa Google kisha chanzo anachokitaka maana yake link zote zitakuja kutoka katika hicho chanzo Mfano inurl:Corona link zote zitakuwa ni za corona.

Wakati huu wa janga la corona kila mtu ana wajibu wa kutafuta taarifa sahihi kutoka katika vyanzo sahihi ili kuweza kupunguza habari za uzushi mtandaoni.