October 7, 2024

Jinsi ya kubaini habari ya uzushi kwenye mitandao ya kijamii

Ukiipata habari hiyo ipuuze au soma kwa makini kabla ya kuchukua maamuzi.

  • Moja ya njia za inayotumika kusambaza habari za uzushi ni kutumia kichwa habari kisichoendana na maudhui ya habari.
  • Ukiipata habari hiyo soma kwa makini kabla ya kuchukua maamuzi. 

Dar es Salaam. Habari za uzushi ni miongoni mambo yanayoisumbua dunia kwa sasa. Wanaopata changamoto zaidi ni wale wanaotumia mitandao ya kijamii. 

Wakati huu ambao dunia inakabiliana na janga la Corona, kasi ya habari hizo za uzushi imeongezeka zaidi na huja kwa namna tofauti.

Ziko aina mbalimbali za habari za uzushi, mojawapo ni ‘False Connection’. 

‘False connection’ ni aina ya habari za uongo ambazo hatumika zaidi kwenye mitandao ya kijamii hasa YouTube na Facebook ambapo kichwa cha habari hutofautiana kabisa na maudhui ya habari yenyewe.

Udanganyifu huo umekua ni njia mojawapo ya kuwavuta watu kusoma vitu wasivyovitaka wanapokua mtandaoni. Mfano, unaweza kukutana na kichwa cha habari kinasema: “Maambukizi ya Corona yaongezeka marudufu Tanzania” huku akiambatana na picha za wagonjwa, lakini ndani ya habari hauwezi kukuta maudhui ya namna hiyo. 


Zinazohusiana:


Mara nyingi madhumuni ya upotoshaji huo ni  kujipatia pesa kwa njia ya matangazo au kujiongezea watazamaji na wasomaji. Lakini hutumika kuharibu heshima na sifa ya watu kwenye jamii.

Ili kukwepa mtego wa habari za namna hiyo hasa zile zinazohusu Corona, ni vema kuzipuuza au kusoma kwa umakini kabla ya kufanya maamuzi ya kutumia au kusambaza kwa watiu wengine. 

Kama kuna jambo utakutana nalo kwenye habari hizo, zipo mamlaka za afya zinazotoa taarifa sahihi kuhusu ugonjwa wa Corona.