October 7, 2024

Jinsi ya kujikinga na Corona unapokua safarini

Ni kuzingatia miongozo ya afya ikiwemo kuvaa barakoa na kunawa mikono kwa maji mara kwa mara.

Dar es Salaam. Kama una mpango wa kusafiri siku za hivi karibuni nje ya nchi kwa ajili ya shughuli mbalimbali  za kibiashara au kikazi, yapo mambo ya msingi ya kuzingatia ili kujikinga na ugonjwa wa Corona.

Miongoni mwa mambo hayo ni kuhakikisha umepima na kupata cheti kitakachithibitisha kuwa hauna maambukizi ya COVID-19 ili kuepuka usumbufu usio wa lazima ukiwa safarini.