Jinsi ya kukabiliana na harufu mbaya ya mdomo
Ni kwa kupiga mswaki walau mara mbili kwa siku na kuepukana na matumizi ya sigara.
- Ni kwa kupiga mswaki walau mara mbili kwa siku na kuepukana na matumizi ya sigara.
- Kupunguza au kuacha kula vyakula vilivyo na sukari nyingi.
Dar es Salaam. Mara nyingi kwa siku ambazo watu wanakuwa hawajapiga mswaki na kusukutua, baadhi yao huwa huogopa kufungua mdomo na kuongea na watu kwa kuhofia harufu mbaya ya kinywa.
Hilo ni jambo la muda mfupi lakini wapo ambao tatizo hilo limewasumbua kwa muda mrefu, licha ya kipiga mswaki kila siku.
Kwa mujibu wa Daktari kutoka hospitali moja Mkoani dar es Salaam, Dk. Theresia Venance, njia sahihi ya kuhakikisha mdomo wako hautoi harufu mbaya ni kudumisha usafi wa kinywa chako ikihusisha fizi, meno na ulimi.
“Baadhi ya watu hufanya zoezi la kupiga mswaki kwa haraka. Wanasugua meno tu, basi! Hali hiyo husababisha kubakiza mabaki ya chakula kwenye fizi na saa zingine ulimi na hapo ndipo harufu mbaya ya mfumo wa kinywa inapoanzia,” amesema Dk Venance.
Hizi ni baadhi ya dondoo ambazo mtu anaweza kuzingatia kuepukana na harufu mbaya mdomoni: