July 5, 2024

Jinsi ya kupata habari za zamani kwenye mitandao ya kijamii

Habari hizo za zamani ni zile zinahusu ugonjwa wa Corona ili kukusaidia kufanya maamuzi hasa kwa wanahabari.

  • Kutafuta taarifa za zamani kwenye mitandao ya kijamii ni jambo linalohitaji ujuzi wa ziada kidogo.
  • Habari hizo za zamani ni zile zinahusu ugonjwa wa Corona ili kukusaidia kufanya maamuzi hasa kwa wanahabari.

Dar es Salaam. Habari iliyokamilika ni ile yenye muendelezo visa na mikasa. Lakini ili muendelezo wa habari ukamilike na kuleta maana kwa walenga ni mpaka muundaaji awe na historia ya jambo husika. 

Hata kuzielewa habari zinazohusu ugonjwa wa Corona, inahitaji kupiga jicho historia yake au habari zilizoandikwa hapo nyuma. Hili linawahusu zaidi wanahabari ambao wako mstari wa mbele kutoa elimu kuhusu janga hilo ambalo linaitesa dunia kwa sasa.

Habari zilikwisha andikwa kuhusu Corona ziko kila mahali mtandaoni, lakini leo nitakufahamisha jinsi ya kutafuta habari za zamani kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook, Twitter na YouTubeili zikuwezeshe kufanya maamuzi. 

Mtandao wa YouTube

Huenda umekuwa ukipata shida kupata video za zamani hasa za corona katika mtandao wa YouTube, lakini nitakuonyesha njia rahisi ya kuzipata. 

Sehemu pekee ambayo unaweza kupata taarifa za YouTube ni kupitia kitafutio cha “Google search”. Unachotakiwa kufanya kama mwanahabri ili kupata video ya zamani  ni sehemu ya zana (tools)  kwenye kitafutio hicho ambapo zinatoa majibu mbalimbali ya muda ambao video husika  ilichapishwa.

Hapo utajipatia video mbalimbali za muda uliokusudiwa kwa ajili ya matumzi yako. Pia hata ndani ya Youtube unaweza kuzipata lakini huenda usizipate zote kama ilivyo kwa Google.

Inawezekana hata Twitter

Changamoto nyingine ya kupata taarifa za zamani ipo kwenye mtandao wa Twitter. Ni ngumu kupata taarifa za nyuma za Twitter ukiwa unatumia Twitter au hata kwa kutumia  kitafutio cha Google bado sio kazi rahisi. 

Mfano ukitaka kupata ujumbe wa kwanza wa Twitter uliotumwa na Waziri wa Afya kuhusu ugonjwa wa corona hutaweza kupata ndani ya Twitter.

Isipo kuwa mwanahabari ataweza kutafuta habari yoyote ya zamani ya Twitter kupitia  zana ya kidijitali ya inayojulikana kama “Twitter Advanced Search functionality

Zana hiyo itakupa majibu yote ya maswali na kukuondolea usumbufu usio wa lazima wa kutafuta habari husika kwenye majukwaa mengine. 

Facebook ni rahisi tu

Zipo hatua tatu muhimu watumiaji wa Facebook wanaosaka habari za zamani kuhusu Corona wanazotakiwa kufuata ili kupata wanachotafuta. 

Hatua ya kwanza ni kuandika neno mojawapo kuhusu habari unayotafuta kwenye kitafutio cha mtandao huo. Hapo utapata kile unachokipata. Kama hujafanikiwa nenda hatua ya pili.

Hatua ya pili  ili kupata  habari hiyo ni kwenda kwenye sehemu ya “Post”. Kisha bonyeza neno Post ambapo utaona vitufe vingine kama vya tarehe, mahali na mtu aliyechapisha habari.

   

Hatua ya tatu utaweza bonyeza kitufe mojawapo ili kuweza kupata taarifa unazozitaka.

Kama bado unasaka habari sahihi kuhusu Corona ni vema kutembele tovuti za afya zinazotambulika ikiwemo Wizara ya Afya ya Tanzania na Shirika Afya Duniani (WHO.