Kampuni ya uwekezaji ya TCCIA yabainisha uwezekano wa kupaa faida mwaka 2018
Mwenyekiti wake wa Bodi ya Wakurugenzi amesema wanatarajia faida baada ya kodi kuongezeka kwa asilimia 49 huku faida kabla ya kodi inatarajiwa kushuka kwa asilimia 44.
TICL ni chombo cha uwekezaji cha TCCIA kilichoanzishwa kwa ajili ya kuiongezea mapato chemba hiyo ili iweze kujiendesha kwa kuwekeza fedha katika kampuni mbalimbali nchini zikiwemo zilizoorodheshwa katika soko la hisa. Picha|Mtandao.
- Mwenyekiti wake wa Bodi ya Wakurugenzi amesema wanatarajia faida baada ya kodi kuongezeka kwa asilimia 49.
- Faida kabla ya kodi inatarajiwa kushuka kwa asilimia 44.
Dar es Salaam. Kampuni ya uwekezaji ya Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA Investment PLC, TICL) imetoa onyo lenye neema kwa wawekezaji wake baada ya kueleza kuwa inatarajia faida baada ya kodi kuongezeka kwa asilimia 49 kwa mwaka ulioishia Desemba mwaka jana ikiwa ni juu zaidi ikilinganishwa na faida ya mwaka 2017.
TICL ni chombo cha uwekezaji cha TCCIA kilichoanzishwa kwa ajili ya kuiongezea mapato chemba hiyo ili iweze kujiendesha kwa kuwekeza fedha katika kampuni mbalimbali nchini zikiwemo zilizoorodheshwa katika soko la hisa.
Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya kampuni hiyo, Fortunatus Magambo inaeleza kuwa ongezeko hilo la faida baada ya kodi linatokana na kuwepo kwa fedha zitokanazo na madai ya kodi (tax credits) zinazohusiana na gawio.
Hata hivyo, Magambo ameeleza kuwa faida ya uendeshaji (operating profit) kabla ya kodi inatarajiwa kushuka kwa asilimia 44 katika mwaka huo ulioishia Desemba 30, 2018 ikilinganishwa na ilivyokuwa mwaka 2017.
“Kampuni inatarajia kuchapisha taarifa za kifedha zilizokaguliwa hivi karibuni,” inasomeka taarifa hiyo ya Magambo iliyochapishwa leo katika tovuti ya Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).
“Wanahisa wanashauriwa kuwa makini wanapokuwa wanauza hisa zao,” imeongeza.
- Maumivu: Bei ya mafuta zapaa
- Mengi kuwekeza Sh68 uchimbaji mafuta, gesi Tanzani
- Mengi alivyoacha alama ya uwekezaji katika teknolojia Tanzania
Kwa mujibu wa taratibu za DSE kampuni zilizojiorodhesha katika soko hilo zinatakiwa kuchapisha onyo kwa wanahisa wake mara tu zitakapojiridhisha kuwa kutakuwa na mabadiliko makubwa katika taarifa zake za kifedha kwa kiwango kisichopungua asilimia 25 ikilinganishwa na mwaka wa awali wa kimahesabu.
Kampuni hiyo iliorodheshwa DSE katika ya Machi mwaka jana, hadi soko linavyofungwa Mei 9 thamani ya hisa moja ilikuwa Sh385. Siku ya kwanza baada ya kujirodhesha katika soko hilo, thamani ya hisa moja ya TICL ilikuwa Sh450.