November 24, 2024

Kicheko kwa wafanyabiashara bei ya maharage ikipanda Dar

Bei ya juu ya gunia la kilo 100 la zao hilo jijini humo ni Sh280,000 katika soko la Tandika kutoka Sh270,000 iliyorekodiwa wiki iliyopita.

  • Bei ya juu ya gunia la kilo 100 la zao hilo jijini humo ni Sh280,000 katika soko la Tandika kutoka Sh270,000 iliyorekodiwa wiki iliyopita. 
  • Wakati bei ya juu mkoani humo ikipanda, pia bei ya chini imepanda pia hadi Sh230,000 kutoka Sh240,000 iliyorekodiwa wiki iliyopita.

Dar es Salaam. Bei ya jumla ya maharage katika jiji la Dar es Salaam imepanda kwa Sh10,000 ndani ya kipindi cha wiki moja, jambo linalowafaidisha zaidi wafanyabiashara na wakulima waliopeleka zao hilo jijini humo.

Takwimu za mazao makuu ya chakula zilizotolewa leo (Mei 4, 2020) na Wizara ya Viwanda na Biashara zinaonyesha kuwa bei ya juu ya gunia la kilo 100 la zao hilo jijini humo ni Sh280,000 katika soko la Tandika.

Hata hivyo, bei hiyo ya juu imepanda kutoka Sh270,000 iliyorekodiwa Jumatatu Aprili 27, 2020 jijini humo katika soko la Tandika.   

Kupanda kwa bei hiyo ya juu kutawanufaisha zaidi wafanyabiashara na wakulima huku wanunuzi wakipoteza wastani wa Sh10,000 kwa kila gunia moja iwapo hesabu hizo zitapigwa kwa viwango vya bei ya juu. 

Bei hiyo iliyotumika wiki iliyopita na leo jiji Dar es Salaam ndiyo bei ya juu ya zao hilo Tanzania Bara kwa mujibu wa takwimu hizo za wizara. 

Wakati bei ya juu mkoani humo ikipanda, pia bei ya chini imepanda hadi Sh230,000 kutoka Sh240,000 iliyorekodiwa wiki iliyopita. 

Aidha, takwimu hizo zinaonyesha kuwa bei ya chini ya zao hilo la chakula inayotumika leo ni Sh105,000 katika Mkoa wa Rukwa.

Endelea kusoma www.nukta.co.tz kwa kwa habari zaidi za takwimu kuhusu bei za mazao, soko la hisa na nyingine za biashara. Kwa habari zaidi Whatsapp +255 677 088 088 au newsroom@nukta.co.tz