November 24, 2024

Kinondoni yaongoza makosa ya jinai Tanzania

Wilaya ya Kinondoni katika jijini Dar es Salaam imetajwa kuongoza kwa kuwa na makosa mengi ya jinai nchini baada ya kurekodi makosa 57,626 kati ya makosa 531,695 yaliyorekodiwa nchi nzima kwa mwaka 2018.

  • Ni baada ya kurekodi makosa 57,626 ambayo ni sawa na asilimia 44.1 ya makosa yote yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  • Kinondoni inafuatiwa na mkoa wa Mwanza ambao una makosa 49,318 yaliyoripotiwa.
  • Makosa ya jinai ambayo yalilipotiwa zaidi ni yale yanahusisha mali za watu, watu na jamhuri.

Dar es Salaam. Wilaya ya Kinondoni katika jijini Dar es Salaam imetajwa kuongoza kwa kuwa na makosa mengi ya jinai nchini baada ya kurekodi makosa 57,626 kati ya makosa 531,695 yaliyorekodiwa nchi nzima kwa mwaka 2018.

Ripoti ya Takwimu Muhimu za Tanzania za 2018 zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), inaeleza kuwa wilaya hiyo inashika nafasi ya kwanza Tanzania kwa makosa hayo yaliyoripotiwa katika kipindi hicho ikifuatiwa na mkoa wa Mwanza ambao ulikuwa na makosa 49,318 yaliyoripotiwa.

Makosa ya jinai ambayo yalilipotiwa zaidi ni yale yanahusisha mali za watu, watu na jamhuri. 

Ripoti hiyo hiyo inaeleza kuwa Kinondoni ndiyo iliyokuwa na makosa mengi zaidi ya mali za watu yaliyofikia 25,397.