November 25, 2024

Kwanini kuna watumiaji wachache wa pasipoti katika huduma za kifedha?

Ni asilimia mbili tu ya watumiaji wa huduma za kifedha waliojiandikisha kutumia huduma hiyo mwaka 2017.

  • Ni watu wawili tu kati ya 100 ama asilimia mbili ya watumiaji wa huduma za kifedha waliojiandikisha hutumia huduma hiyo.
  • Watumiaji wa vitambulisho vya kupigia kura ni wengi kuliko vitambulisho vyingine.

Dar es Salaam. Je wewe ni mtumiaji wa pasipoti katika kujiandikisha kwenye huduma za kifedha? Kama ndiyo basi utaingia katika kundi la wachache wanaoitumia pasipoti zao katika kujisajili na huduma hizo .

Hayo yamebainika katika Ripoti ya utafiti wa masuala ya kifedha ya Finscope ya mwaka 2017  FinScope Tanzania 2017 kuliofanywa ati ya Aprili-Julai unaeonyesha kuwa katika fomu wanazopewa wateja kujaza na watoa huduma za fedha wakati wa usajili huwa wanaweka vitambulisho mbalimbali kama alama ya utambulisho.

Ripoti hiyo imeonyesha kuwa katika kufanikisha huduma hizo za kifedha, zaidi ya robo tatu ya watumiaji ama asilimia 83 hutumia vitambulisho vya kura huku asilimia tisa hutumia vitambulisho vya Taifa. Hii ina maana kuwa zaidi ya watumiaji wanane kwa 10 hutumia vitambulisho vya kura kufanya miamala yao huku takriban mmoja tu kati ya 10 hutumia vitambulisho vya Taifa.

Ripoti hiyo inaeleza zaidi kuwa asilimia tatu ya watumiaji hao hutumia vitambulisho vya TASAF (Mfuko wa maendeleo ya Jamii), leseni za udereva (asilimia tano) huku wanaotumia pasipoti katika kufanikisha miamala yao huwa ni asilimia mbili tu.

Takwimu hizi zina maana gani? Ni kweli watanzania wenye pasipoti ni wachache au hawapendi kutumia katika kujiandikishia kwenye huduma mbalimbali za kifedha?