October 7, 2024

Kwanini tatizo la kupoteza kumbukumbu linawakumba vijana?

Baadhi ya tabia walizo nazo vijana ndiyo sababu ya wao kukutwa na changamoto hii.

  • Sababu kubwa inachochewa na baadhi ya tabia za kimtindo maisha walizo nazo vijana.
  • Wengi hushindwa kukumbuka vitu vidogo vidogo ikiwemo katika matumizi ya simu  na uhifadhi.

Dar es Salaam. Hivi karibuni nilipata nafasi ya kuzungumza na rafiki yangu wa karibu sana, Nilikuwa nikimkosoa juu ya kukosa kumbukumbu na kushindwa kutimiza ahadi anazoahidi.

Kujitetea, rafiki huyo aliamu kuvunja ukimya na kuniambia kuwa amekuwa akisumbuliwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu hasa katika vitu vidogo vidogo ikiwemo katika kutumia simu na sehemu anazohifadhi vitu vyake.

“Unaweza kukuta nimefungua “WhatsApp” kumtumia meseji mtu, nikiifungua nakua nimesahau nani nilidhamiria kumtumia ujumbe na ni ujumbe gani. 

Leo tu nimechana nywele na sikumbuki wapi nimeweka chanuo langu,” amesema rafiki yangu huyo.

Hata hivyo, hakuwa mtu wa kwanza kunielezea tatizo hilo hivyo niliona umuhimu wa kumtafuta mtaalamu ili anipatie suluhu juu ya tatizo hilo.

Daktari kutoka Hospitali ya Shree Hindu Mandal, Dk Frank Minja ameiambia Nukta Habari (www.nukta.co.tz) kuwa tatizo hilo ni matokeo ya sababu mbalimbali ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya na pombe kali. 

Kufahamu zaidi, tazama video hii: