October 6, 2024

Mabalozi tisa wawasilisha hati za utambulisho Ikulu Dar

Rais John Magufuli amepokea hati za utambulisho mabalozi wateule tisa walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini Tanzania wenye makazi yao nje ya nchi ili kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia.

  • Zimepokelewa na Rais John Magufuli leo.
  • Ni mabalozi wateule walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini Tanzania wenye makazi yao nje ya nchi.
  • Baada ya kupokea hati hizo, Rais amefanya na mazungumzo na kila balozi mteule. 

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amepokea hati za utambulisho mabalozi wateule tisa walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini Tanzania wenye makazi yao nje ya nchi ili kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia.  

Rais Magufuli amepokea hati hizo leo (Januari 28, 2020) Ikulu jijini Dar es Salaam, ambapo mabalozi hao wamewasilisha hati hizo kwa nyakati tofauti. 

Balozi mteule wa Ureno nchini Tanzania mwenye makazi yake nchini Msumbiji, Maria Amelia Mario De Paiva ndiye aliyekuwa wa kwanza kuwasilisha hati yake ya utambulisha na kufuatiwa na Balozi mteule wa Singapore nchini mwenye makazi yake nchini Singapore, Douglas Foo Peow Yong.

Wengine ni Alex Chua ambaye ni Balozi mteule wa Ufilipino nchini mwenye makazi yake chini Kenya, Angela Veronica Comfort, Balozi mteule wa Jamaica nchini mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini na Dk Christian Fellner, Balozi mteule wa Austria  nchini mwenye makazi yake nchini Kenya.


Soma zaidi: 


Mabalozi wengine ambao wamewasilisha hati zao ni pamoja na  Balozi mteule wa Ghana nchini mwenye makazi yake nchini Kenya, Fransisca Ashiete Odunton na Balozi mteule wa Venezuela nchini mwenye makazi yake nchini Kenya,Jesus Agustin Manzanila Puppo. 

Yacin elmi Bouh anakuwa Balozi mteule wa Djibouti nchini mwenye makazi yake nchini Kenya na Oded Joseph anakuwa Balozi mteule wa Israel nchini mwenye makazi yake nchini Kenya 

Hafla hiyo ya kuwasilisha na kupokea hati za utambulisho imefanyika fanyika Ikulu Jijini Dar es salaam ambapo Rais Magufuli baada ya kupokea hati hizo amefanya na mazungumzo na kila balozi mteule.