October 7, 2024

Madhara yanayoambatana na kumeza dawa bila kushauriwa na daktari

Ni pamoja na kukomaza ugonjwa kwani kumeza dawa bila maelekezo ya daktari kunazuia dalili na siyo kutibu ugonjwa.

  • Ni pamoja na kukomaza ugonjwa kwani kumeza dawa bila maelekezo ya daktari kunazuia dalili na siyo kutibu ugonjwa.
  • Pia, mfululizo wa tabia hii hupelekea mwili kuwa sugu kwa baadhi ya dawa.

Dar es Salaam. Ni mara nyingi watu wamekua wakinunua dawa za kutuliza maumivu baada ya kupatwa na homa au kichwa kuuma.

Hata baada ya kufanya hivyo, ni watu wachache hukumbuka kwenda hospitali kwa ajili ya kufanya uchunguzi kubaini ni kipi hasa kinachowasumbua.

Hali hiyo imekua ni tabia kwa baadhi na kupelekea watu kujinunulia dawa au kumeza zile zilizowahi kubaki hapo awali bila hata ya kupata ushauri wa mtaalamu wa afya.

Dk Beno Nkwama kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ameiambia Nukta Habari (www.nukta.co.tz) kuwa magonjwa mengi huonyesha dalili  kama kichwa kuuma, homa, kuharisha na hata kutapika na hivyo kumeza dawa bila ushaur wa daktari siyo salama.

Ni madhara gani yanayoambatana na tabia hiyo, tazama video hii kujifunza