July 8, 2024

Maisha mtelezo kwa wana Iringa

Mkoa wa Iringa viazi mviringo vinauzwa kwa Sh50,000 kama bei ya juu zaidi na ya chini zaidi huku mkoani Mtwara gunia kama hilo likiuzwa kwa Sh120,000

  • Ni baada ya mazao yote ya  chakula  kuuzwa chini ya Sh 200,000.
  • Mkoani humo viazi vinauzwa kwa Sh50,000 wakati wakazi wa Mtwara wanatoa Sh120,000 kununua gunia hilo hilo.
  • Iringa ni kati ya mikoa inayouza gunia la maharage kwa bei ya nchini.

D​ar es Salaam. Iringa ni kati ya mikoa yenye ahueni kimaisha kwa siku ya  leo ikiwa ahueni hiyo itapimwa kwa bei ya kununulia  mazao ya chakula.

Kwa mujibu wa bei za mazao zilizotolewa leo na Wizara ya Viwanda na Biashara, wakazi wa mkoa huo watanunua zao lolote kwa bei isiyozidi Sh 200,000.

Mazao maarufu ya chakula yakiwemo maharage, mchele, viazi mviringo na mahindi yatauzwa kwa  bei chini ya Sh190,000 ikilinganishwa na mikoa mingine kama Dar es Salaam ambayo kwa leo, gunia la maharage litauzwa  kwa Sh250,000 kama bei ya juu zaidi kwenye Soko la Temeke wakati Iringa likiuzwa Sh180,000 kama bei ya juu zaidi.

Kwa iringa, gunia la maharage lenye kilo 100 limeuzwa kwa Sh150,000 kama bei ya chini zaidi ikiwa ni sawa na bei illiyorekodiwa Julai 3, 2020.

Pia, Mkoa wa Iringa viazi mviringo vinauzwa  kwa Sh50,000 kama bei ya juu zaidi na ya chini zaidi huku mkoani Mtwara gunia kama hilo likiuzwa kwa Sh120,000 na Sh100,000 ikiwatoka wakazi wa Mkoani Katavi.

Gunia la  mahindi halijavuka Sh50,000 kama mikoa mingine ikiwemo Mwanza ambapo gunia la kama hilo linanuzwa kwa Sh80,000 wakati wa  wakazi wa Manyara wa kinunua  kwa Sh72,000.

Huku  gunia la mchele likiuzwa kwa Sh180,000 kama bei ya juu zaidi ambayo ni pungufu ya Sh30,000 ikilinganishwa na Dar es Salaam  katika Soko la Ilala ambapo zao hilo linanunuliwa kwa Sh210,000 kama bei ya juu zaidi ukilinganisha na  mikoa ya Tabora, Manyara na Njombe ambayo  gunia hilo linauzwa  kwa Sh200,000.