November 24, 2024

Makosa matano yanayowasumbua wajasiriamali

Kati ya vitu ambavyo wajasiriamali wanapaswa kuviepuka ni pamoja na hofu ya kutaka kumridhisha kila mtu.

  • Ni pamoja na kukataa kujiendeleza kielimu.
  • Wengine wanataka kumridhisha kila mtu na hivyo kukosa dira.
  • Unashauriwa kuwekeza kwenye kujifunza njia bora za kufanya biashara yako

Dar es Salaam. Kuanzisha biashara kama mjasiriamali ni hatua moja lakini kuiendeleza biashara hiyo ili izidi kukupatia kipato ni hatua nyingine ambayo inahitaji uthubutu, kujifunza na kukubali kuachilia baadhi ya itikadi zako za kibiashara pale zinapokuwa hazifanyi kazi.

Hata hivyo, kutokana na uoga na kukataa kuthubutu, wanaendelea kupiga hatua moja mbele na moja nyuma na kubaki palepale walipoanzia.

Tovuti ya masuala ya ujasiriamali ya entreprenoria.com imesema kati ya vitu ambavyo wajasiriamali wanapaswa kuviepuka ni pamoja na hofu ya kutaka kumridhisha kila mtu na kulipotezea wazo la biashara kwa kuogopa mtazamo ambao watu wanaweza kuwa nao juu yako.

Kama unauhakika na unachokifanya na umefanya utafiti wa kutosha, unahitaji uthubutu wa kufanya jambo hilo huku ukiwekeza kila tone la nguvu yako kuona linafanikiwa. 

Makosa ya wajasiriamali wengi yapo katika video hii fupi. Tafadhali tazama.