October 7, 2024

Mambo ya kufahamu kuhusu chanjo ya Covid-19

Ni pamoja na chanjo hiyo kutokuwafaa watu wenye mzio na wanaoishi na magonjwa ya kudhoofisha kinga ya mwili.

Dar es Salaam. Mengi yanazungumziwa kuhusu chanjo ya Covid-19 yakiwemo muda ambao umetumika katika kutengeneza chanjo hiyo ikilinganishwa na chanjo ya magojwa mengine yanayosababishwa na virusi ukiwemo Ukimwi.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeeleza kuwa chanjo ya Covid-19 inayoendelea kutolewa katika baadhi ya nchi duniani inaambatana na masharti kwa kuwa chanjo hiyo haiwezi kumfaa kila mtu.

Katika andiko la WHO linalozungumzia namna chanjo hiyo inavyofanya kazi, shirika hilo limesema chanjo hiyo isitolewe kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi na wale wenye saratani.

Hata hivyo, watu hao bado wanaweza kubaki salama pale watakapoishi miongoni mwa jamii iliyopewa chanjo.

Jifunze zaidi kwa kutazama video hii.