October 7, 2024

Mambo yatakayokusaidia kutunza chakula nyumbani

Ni pamoja na kutumia njia sahihi za kuhifadhi na kununua chakula kulingana na mahitaji ya familia.

  • Ni pamoja na kutumia njia sahihi za kuhifadhi na kununua chakula kulingana na mahitaji ya familia.
  • Kama una chakula kingi, gawa kwa watu wenye uhitaji.

Dar es Salaam. Ugomvi baina ya akina mama wa nyumbani na wasaidizi wao wa kazi ni kutupa chakula hasa kinapokuwa kimeharibika kwa sababu hakijatumika au kimekaa muda mrefu.

Hali hiyo huzua tafrani ikizingatiwa kuwa chakula hununuliwa kwa fedha ili kitumike na watu. 

Hata hivyo, zipo sababu mbalimbali zinazosababisha chakula kuharibika na kutupwa hata kabla hakijatumika ikiwemo kununua chakula kingi kwa wakati mmoja na kukosa njia sahihi za uhifadhi. 

Ufanye nini kuzuia uharibifu wa chakula nyumbani? Tazama video hii.